Na Woinde Shizza-Globu ya jamii

IDARA ya uhamiaji mkoani Kilimanjaro imemfukuza nchini raia wa Kenya Magdalena Wavinya (43)ambaye ni Mkazi wa kijiji cha Ghona katika kata ya Kahe Mashariki wilayani Moshi Vijijini ,mkoani humo kwa kosa la kuishi nchini kwa zaidi ya miaka 20 kinyume cha sheria.

Aidha inamshikilia mumewe ,Steven Mrutu(45)kwa madai ya kuwa na mashaka na uraia wake, pamoja na Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Mikameni wilayani humo Panaska Issa Manyi anayedaiwa kuishi na mwanamke ,Lyidia Nakiete raia wa Kenya ambaye alitoroka muda mfupi wakati maofisa wa uhamiaji wakimfuatilia kwa ajili ya vibali vya makazi.

Akizungumza leo Machi 19,2019 na ofisini kwake Ofisa Uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro Albert Rwelamira alisema idara hiyo imelazimika kumfutia kibali cha muda anachotumia mkazi huyo na kumpatia saa 24 awe ameondoka nchini tangu Machi 15,mwaka huu

"Tumelazimika kumfukuza nchini Magdalena kwa sababu kubwa mbili yakwanza amekuwa akiishi nchini kwa zaidi ya miaka 20 bila kuwa na kibali , tangu mwaka 2017 kwa maana amekuwa akikata paspoti ya miezi mitatu na pindi muda wake unapomalizika hurejea nchini Kenya na kukata nyingine ya muda huo na kurudi hapa nchini, ’’amesema

Aliongeza sababu nyingine ni kuidanganya idara hiyo kuwa ana cheti cha ndoa aliyofunga na mumewe, Steven Mrutu mwaka 2003 ,katika Kanisa Katoliki lililopo Himo mkoani humo, lakini idara hiyo ilifuatilia na kubaini kwamba hakuna jina hilo katika orodha ya watu waliofungwa ndoa kanisani hapo.

Pia alifafanua kushikiliwa kwa Mrutu ni kutokana na uraia wake kuwa na mashaka kwani mwaka 2017 alikamatwa na kutakiwa kuleta vielelezo vya uraia wake lakini hakuwahi kufanya hivyo,ila idara hiyo ilifuatilia mahala alipodai alisoma ikiwemo shule ya msingi kisimani aliyosoma mwaka 1986 ambapo uongozi wa shule hiyo ulitoa orodha ya wanafunzi waliotahiniwa mwaka huo jina lake halikuwepo.

Akizungumzia kadhia hiyo,Magdalena alilalamikia hatua ya kufukuzwa nchini kwani ameishi kwa zaidi ya miaka 20 na kufanikiwa kuzaa watoto watano wanaosoma katika shule mbalimbali nchini,hivyo kitendo cha kumfukuza na kuendelea kumshikilia mumewe ni kuwafanya watoto wake waishi maisha ya taabu na kuiomba serikali ya Tanzania imwonee huruma kwani maisha yake yote amewekeza hapa nchini.

Awali baba mzazi wa Mrutu,Awadhi Mrutu alidai kuwa Mkazi wa Makuyuni  wilaya ya Moshi vijijini,alisema wakati akifanya kazi za udereva wa malori makubwa kwenye nchi jirani na mikoani alibahatika kukutana na mama yake aitwaye Amina Rashird na kubahatika kupata ujauzito ambapo mwaka 1975 alijifungua mtoto huyo aitwaje Stivini .

Mzee huyo mwenye watoto nane aliowazaa nje ya ndoa ameilalamikia idara hiyo kwa kumtuhumu na kumkamata mara kwa mara mwanaye kwa madai kwamba si raia wa Tanzania jambo alilosema ni uonevu mkubwa kwani yeye kama baba mzazi bado yupo hai na kama wanahitaji vielelezo vyovyote ikiwemo kupima vina saba wamfuate yeye na yupo tayari muda wowote.

Ameitaka idara hiyo ya uhamiaji kumpeleke mahakamani mwanaye na kuacha kumkamata na kumshikilia kituo cha polisi huku wakimnyima dhamana kwa kuwa ni kinyume cha sheria.

 Afisa uhamiaji Wa Mkoa Wa Kilimanjaro Albert Rwelamira akizungumza na na waandishi Wa habari (Picha na Woinde Shizza globu ya jamii Arusha)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...