Na Woinde Shizza Globu ya Jamii.

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limetambulisha mfumo mpya wa ukusanyaji wa Madeni ya Makosa ya usalama barabarani unaotumia kamera maalumu zenye uwezo wa kupiga picha na kutambua gari linalodaiwa.

Akizungumza na vyombo vya habari mapema leo Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Arusha Jonathan Shana amesema kuwa mfumo huo mpya utarahisisha kutambua Magari yote yanayodaiwa kupitia kamera maalumu zilizofungwa barabarani zitakazo kuwa zikipiga picha na kuonyesha kiasi ambacho gari linadaiwa.

Kamanda Shana amesema kuwa Jiji la Arusha limepata  kamera tatu za kisasa zinazotembea na zimefungwa katika maeneo mbalimbali katika Jiji la Arusha na kwamba machine hizo zinauwezo wa kutambua  namba za Magari ya aina mbali mbali.

Mtaalamu wa kitengo cha IT kutoka makao Makuu ya jeshi la polisi nchini,ACP Mayala Towo amesema mfumo huo umeanza kutumika  jijini dar es salaam tangu mwaka 2015, na sasa unasambaa nchi nzima na lengo ni kuhakikisha fedha ya serikali zinakusanywa kwa wakati.
Mmoja ya askari wa usalama barabarani anayeendesha mfumo huo wa kamera, Pc Masalu Yamala amesema zoezi hilo limekuwa na mafanikio makubwa kwani imerahisisha utambuzi wa Magari yanayodaiwa tofauti na hapo awali kwa kuwa lilikuwa likipoteza muda mwingi.

kamanda Shana alitumia wasaa huo kujitambulisha kwa waandishi wa habari na kueleza vipaumbele vyake vya utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kupambana na uingizaji na utumiaji wa Dawa za kulevya ikiwemo Cocaine, Mirungi na Bangi.7

Picha ikionyesha Mmoja ya askari wa usalama barabarani anayeendesha mfumo huo wa kamera, Pc Masalu Yamala akiwaonyesha waandishi  Wa habari na wananchi jinsi kamera hiyo inavyofanya Kazi(Picha na Woinde Shizza globu ya jamii ).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...