Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

SHIRIKA la Jukwaa la Utu wa  Mtoto (CDF) limeandaa kongamano la kitaifa kujadili hali ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kutokomeza na kuboresha upatikanaji wa viwango vya huduma kwa waathirikia wa vitendo vya ukatili.

Kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika Machi 21 na22 linatarajia kujadili namna ya kutokomeza vitendo vya ukatili yakidhaminiwa na Ubalozi wa Uswidi.

Mkurugenzi wa CDF Koshuma Mtengeti amesema kuwa Kongamano hilo litafungiliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  na kuhudhuriwa na wageni takribani 600 kutoka mataifa mbalimbali.

Mtengeti amesema, lengo kuu la kongamano hilo ni kuwapatia fursa viongozi wa kitaifa, watafiti, asasi za kiraia, wanataluma, viongozi wa dini, wanaharakati wa haki za binadamu, wadau wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi kujadili hali halisi ya ukatili pamoja na namna ya kuimarisha mikakati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“ Kongamano hili litaangazia mada kuu sita ambazo ni halinya ukatili kwa watoto katika familia na mashuleni, ukatili wa kijinsia na unyanyasaji, mimba na ndoa za utotoni, ukeketaji, malezi katika ulimwengu wa kisasa, ukatili wa kingono, ukatili dhidi ha watoto kwenye mitandao na namna ya kuwapatia msaada wahanga wa vitendo hivyo,” amesema Mtengeti.

“Tanzania inakabiliwa na kiwango cha juu cha ukatili kwa wanawake na watoto ikiwemo vipigo, mimba na ndoa za utotoni, ukeketaji, unyanyasaji na hata ukatili wa kingono licha ya juhudi  kubwa zinazofanywa kupingana na vitendo hivyo na nchi yetu imekuwa ikijaribu kutekeleza mpango wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ,”amesema.

Mtengeti ameeleza kuwa kwa mujibu wa demografia ya afya mwaka 2015/16 inaonyesha kuwa idadi ya wasichana wanaopata watoto katika umri wa miaka 15-19 imeongezeka na kufikia asilimia 27 kutoka asilimia 23 mwaka 2010, asilimia 40 ya wanawake wa umri wa miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15.

Ameeleza, kwa mujibu wa ripoti ya ukatili dhidi ya watoto iliyotayarishwa na UNICEF 2011 ilibainisha kuenea kwa aina za ukatili wa kijinsia, kimwili na kiakili nchini Tanzania dhidi ya watoto na kuonyesha kuna asilimia 28 ya wasichana na asilimia 13 ya wavulana wamefikiwa na ukatili wa kijinsia kabla ya kutimiza miaka 18, na zaidi ya asilimia 70 ya wasichana na wavulana wamefanyiwa ukatili wa kimwili na zaidi ya robo wametndewa ukatili wa kiakili.

Mhadhiri Chuo Kikuu Kishirikishi (DUCE) Dr Mabula Nkuba amesema kongamano hili litatoa mwanga wa namna ya kupambana na kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto na wao kama wazazi, walezi na walimu wameamua kushirikiana na CDF kuunga mkono jitihada hizo na ukiangalia matukio ya ukatili wa kimwili ni mengi zaidi kuliko ukatili wa kijinsia kulingana na tafiti ya mwaka 2011.

Ripoti mbalimbali za haki za binadamu zimeweza kuonyesha kuna ongezeko kubwa la ukatili dhidi ya watoto kwa kipindi cha mwaka 2018 ukilinganishwa na mwaka 2017 nchini.

Aidha, kongamano hilo litatoa fursa kwa washiriki kudadavuabukubwa wa sura za ukatili yanayowasibu wanawake na watoto  na litasaidia juhudi za kuweka mikakati madhubuti ya kuzuia, kukabili na kuanzisha utaratibu wa kuboresha huduma kwa watoto na wanawake waathirika wa ukatili.
 Mkurugenzi wa Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Koshuma Mtengeti akizungumza na waandishinwa habari kuelekea kongamano la kitaifa la kujadili hali ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto  litakalofanyika Machi 21-22 Mwaka huu Jijini Dar es Salaam na Mgenj rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishirikishi DUCE Dr Mabula Nkuba akielezea kongamano la kujadili hali ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na namna wadau watakavyodadavua  kwa ukubwa wa sura za ukatili unavyowasinu wanawake na watoto katika jamii inayotuzunguka hapa nchini, kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Koshuma Mtengeti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...