Ni ajabu namna ambavyo simu ya mkononi ilivyobadili maisha ya kila siku ya binadamu. Miongo kadhaa iliyopita, simu ilionekana kama kifaa cha anasa ambacho watu wachache wenye uwezo wa kifedha ndiyo walikuwa wanamiliki.
Lakini leo hii, simu ya mkononi imekuwa ni kifaa muhimu ambacho asilimia kubwa ya binadamu hawawezi kufanya shughuli zao bila ya kuwa nacho. Simu haitumiki tena kwa matumizi ya kupiga na kupokea simu au kutuma na kupokea ujumbe mfupi wa maneno bali ni kifaa ambacho kinarahisisha shughuli kadha wa kadha za maisha ya kila siku ya binadamu.

Kupitia simu ya mkononi mtu anaweza kupata huduma za intaneti - kutumia barua pepe, kupata habari, kuperuzi mitandao ya kijamii, huduma za kibenki, kulipia huduma tofauti, kufanya manunuzi ya bidhaa kwa njia ya mtandaoni, kusikiliza muziki, kutazama video, burudani na masuala chungu mzima ambayo yanazidi kuvumbuliwa kadri siku zinavyosonga mbele.

Kutokana na umuhimu wa simu ya mkononi kumekuwepo na ongezeko kubwa la idadi ya watumiaji wa simu duniani. Kwa mujibu wa takwimu zilizopo kwenye mtandao wa GSMA, watumiaji wa simu duniani wamefikia zaidi ya bilioni 5. Hii inamaanisha kwamba zaidi ya nusu ya watu duniani, ambayo ni zaidi ya bilioni 7.5, wanatumia simu katika shughuli zao za kila siku.

Tanzania nayo haiko nyuma katika matumizi ya simu za mkononi. Ikiwa na watu zaidi ya milioni 54, idadi ya wananchi wanaotumia simu za mkononi inazidi kuongezeka kila mwaka. Hivi sasa, ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya watumiaji wa simu za mkononi katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Kwa mujibu wa ripoti ya Takwimu za Mawasiliano iliyotolewa na TCRA ya kuanzia mwezi Oktoba mpaka Desemba 2018, inaonyesha kwamba idadi ya watumiaji wa simu wameongezeka na kufikia zaidi ya milioni 43 mwaka 2018 kutoka milioni 40 mwaka 2017. Hii ni sawa na ueneaji wa asilimia 81 ya Watanzania wanaotumia huduma za simu za mkononi nchini.



Ongezeko la umiliki na utumiaji wa simu za mkononi linasababishwa na sababu kadhaa zikiwemo; ongezeko la makampuni ya mitandao ya simu - ambayo yamepelekea unafuu kwenye upatikanaji wa huduma za mawasiliano, vifurushi vya mtandao wa intaneti pamoja na huduma za kifedha, ongezeko la makampuni yanayouza simu - ambayo yamepelekea simu za mkononi kupatikana kwa urahisi na bei nafuu miongoni mwa Watanzania wengi.

Katika kuhakikisha watumiaji na wamiliki wa simu za mkononi wanazidi kuongezeka, Jumia imekuwa mstari wa mbele katika kurahisisha upatikanaji wake kwa kuwaunganisha wauzaji na wanunuzi kwa njia ya mtandaoni. Njia hii itawapatia uwanja mpana wateja kunufaika kwa kuweza kuperuzi maelfu ya bidhaa za simu kutoka kwa wauzaji mbalimbali wa simu mtandaoni, kununua na kupelekewa mpaka mahali walipo.
Kila mwaka, Jumia huwa na kawaida ya kuwa na kampeni kubwa ya mauzo ya bidhaa za simu pekee kwa muda wa wiki nzima! Wakati wa kampeni hii, wateja hufurahia mauzo ya simu za aina zote kwa gharama nafuu, kupatiwa punguzo kubwa la bei, vocha za bure za manunuzi, pamoja na kuzawadiwa zawadi lukuki pindi wanapofanya manunuzi yao ya kila siku.

Zimebaki siku chache kabla ya kampeni hii kutangazwa na kuanza rasmi. Kwa sasa, unaweza kutembelea mtandao wa Jumia kujionea bidhaa zilizopo huku ukifuatilia kwa ukaribu kurasa zake za mitandao ya kijamii kupata taarifa mbalimbali. Usicheze mbali, kaa mkao wa kula!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...