Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii wakipewa maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka, Hashimu Paschal kuhusiana na matumizi ya silaha za moto aina ya AK-47 i wanapofanya doria wakiwa Hifadhini wakati wajumbe wa kamati hiyo ya Bunge walipotembelea chuo hicho mjini Moshi. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Shabani Shekilindi (wa pili kulia) akiwa na Wajumbe wa Kamati hiyo wakipewa maelezo huku wakiangalia baadhi ya taswira za wanyamapori mbalimbali wanaotumika kwa ajili ya kuwafundishia wananfunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro wakati kamati hiyo ilipofanya ziara Chuoni hapo.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii wakipewa maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka, Judith Mwela kuhusiana na handaki lililotengenezwa na kabila la Wachaga mnamo karne ya 18 kwa ajili ya kujihami dhidi ya maadui kabla ya Wajumbe hao kuingia ndani ya Handaki hilo kwa ajili ya kujionea , Handaki hilo lipo katika Chuo hicho

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Shabani Shekilindi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na watumishi wakati kamati hiyo ilipofanya ziara katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Shabani Shekilindi akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwasalimia na baadhi ya Watumishi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara Chuoni hapo.

Baadhi ya magari maalum yAnayotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka wakati wanapofanya mafunzo kwa vitendo katika Hifadhi nchini. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII) 

…………………………………………………………………………………………
Wizara ya Maliasili na Utalii imesema imeanza kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto zinazokikabili Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka ili kiendeleze hadhi yake ya kuwa Chuo cha Kimataifa. 

Hatua hiyo inakuja kufuatia kupungua kwa idadi ya wanafunzi wa kigeni wanaojiunga na Chuo hicho kila mwaka. 

Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii iliyotembelea Chuo hicho mkoani Kilimanjaro, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema shabaha ya Wizara ni kukiona chuo hicho kikiendelea kuwa na hadhi ya Kimataifa. 

Amewaeleza Wajumbe hao kuwa hatua zilizochukuliwa ni pamoja na Wizara kuendelea kufanya mazungumzo na vyombo vya udhibiti na Usimamizi wa Elimu hapa nchini ( TCU na NACTE) ili viangalie namna ya kuondoa masharti magumu yanayosababisha baadhi ya masomo yanayotolewa na nchi nyingine yasitambuliwe chuoni hapo. 

Mhe.Kanyasu ameiambia kamati hiyo kuwa sababu nyingine ya idadi ya Wanafunzi wa kigeni kupungua ni baadhi nchi kama Malawi na Kenya kuanzisha vyuo vyao tofauti na ilivyokuwa mwanzo. 

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Shabani Shekilindi amesema Chuo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za uhaba wa wahadhiri pamoja na uchakavu wa miundombinu. 


Amesema kupitia Kamati anayoiongoza atahakikisha kuwa changamoto zote zinapatiwa majibu ili chuo hicho kiendelee kutoa huduma bora. Amekishauri chuo hicho kiendelee kuzitangaza kozi zake ndani na nje ya nchi. Naye Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Boniphace Getere amekishauri chuo hicho kiingie mkataba na watu binafsi kwa ajili kujenga mabweni yatayokayosaidia kutatua changamoto ya wanafunzi 228 kati ya 600 wanaolazimika kupanga nyumba nje ya Chuo hicho.
Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori , Mweka kilianzishwa mwaka 1963 kikiwa na wanafunzi 25 kutoka Kenya, Uganda Malawi , Cameroun na Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...