Na Estom Sanga- Mtwara 

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wameridhishwa na mafanikio ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF ambao umeleta hamasa kubwa kwa Walengwa wake kupambana na umaskini. 

Wajumbe wa Kamati hiyo ambao wametembelea kijiji cha Namela katika wilaya ya Mtwara ambako wamepata fursa ya kuonana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kushuhudia namna Walengwa hao wanavyotumia fursa za Mpango huo kujiletea maendeleo. 

Wakiwa kijijini hapo Wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wamepata ushuhuda kutoka kwa baadhi ya Walengwa wa TASAF ambao wametumia fursa ya kuwepo kwenye Mpango huo kwa kuanzisha miradi midogo midogo ya ufugaji wa mbuzi na Kuku wa Kienyeji kuhamasisha watoto wao kuhudhuria masomo huku wengine wakiboresha makazi yao na kununua vifaa vya umeme jua ( solar systems. 

‘’…….nimetumia fursa ya kuorodheshwa na TASAF kwa kununua mbuzi ambapo hadi sasa nina zaidi ya mbuzi kumi” ninaishukuru sana serikali kwa kuniwezesha kujikomboa amesisitiza mmoja wa walengwa mbele ya Wajumbe wa Kamati hiyo ya bunge. 

Taarifa ya mkoa wa Mtwara imeonyesha kumekuwapo na manufaa ya kujivunia ambayo yamepatikana kutokana na utekelezaji wa shughuli za TASAF mkoani humo hususani katika sekta za Afya, Elimu,Miundombinu,uundaji wa vikundi vya kuweka na kuwekeza akiba na kujiongezea kipato kwa kuanzisha shughuli za kiuchumi. 

Walengwa hao wa TASAF mkoani Mtwara pia wamehamasishwa kuunda vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana vipatavyo 3,070 vyenye jumla ya wanachama 43,872 ambapo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka uliopita vikundi hivyo vimefanikiwa kujiwekea akiba ya zaidi ya shilingi milioni 537 na kukopeshana kiasi cha shilingi milioni 409 kwa ajili ya kuwekeza kwenye shughuli za kiuchumi hususani kilimo na ufugaji. 

Akizungumza kwa niaba ya Wajumbe wa Kamati hiyo Mwenyekiti wake Mheshimiwa Steven Rweikiza amepongeza mafanikio yaliyopatikana katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuwapunguzia Wananchi na adha ya umaskini kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF. 

Hata hivyo kilio kikubwa ambacho kimekuwa kikipazwa sauti na Wajumbe wa Kamati ,Viongozi na Wanachi kwenye maeneo mengi nchini ni sehemu ya Wananchi ambao bado wanaishi kwenye hali ya umaskini ambao bado hajapata fursa ya kujumuishwa kwenye huduma za Mpango wa Kunusuru Kasya Maskini. 

Kwa nyakati tofauti Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Kapteini Mstaafu George Mkuchika amekuwa akisisitiza azma ya serikali ya kuhakikisha kuwa katika utekelezaji wa sehemu ya pili ya Mpango wa kunusuru kaya maskini vijiji /shehia na wananchi ambao watakidhi vigezo vya kuorodheshwa kwenye Mpango wanapata fursa hiyo . 

 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya bunge ya kudumu ya bunge ua utawala na serikali za mitaa wakifurahia maelezo baadhi ya Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Namela mkoani Mtwara.
 Mmoja wa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe.Venance Mwamoto (aliyevaa shati jeupe) na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga aliyenyoosha mkono wakiwa na mmoja wa Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Namela wilaya ya Mtwara mbele ya nyumba aliyoijengwa kwa kutumia fursa za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. 
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya kudumu ya Utawala na serikali za mitaa Mhe. Steven Rweikiza (mwenye Kaunda suti) akiwasikiliza  Walengwa wa TASAF wakielezea mafanikio waliyoyapata baada ya kujumuishwa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Namela mkoani Mtwara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...