JOSEPH MPANGALA , NACHINGWEA LINDI

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za mitaa imekabidhi hati za Kimila za Umiliki ardhi Mia Moja{100} kwa wakazi wa kijiji cha Mbondo kilichopo Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi 

Ugawaji wa Hati hizo unakuja baada ya kujengewa Uwezo na Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania{MKURABITA} kwa kutoa mafunzo jinsi ya kupima ardhi kwa Halmashauri ya Nachingwea kwa lengo la kuongeza thamani ardhi hizo pamoja na kuondokana na Migogoro Mbalimbali inayotokana na Mipaka.

Menyekiti wa kamati hiyo Jason Rweikiza amesema ugawaji wa Hati utawezesha wakulima kuweza kukopa katika taasisi mbalimbali za kifedha kwa lengo la kuendeleza ardhi hizo kwa kulima kilimo kitakacholeta tija na mafanikio na hivyo kujiletea maendeleo.

“Tayari taasisi za kifedha zimeanza kukubali kupokea Hati hizi hivyo wakulima wananafasi kubwa ya kuweza kuendeleza mashamba yao kwa kulima kisasa zaidi na kujiletea maendeleo”amesema Rweikiza mwenyekiti wa kamati.

Naye Mratibu wa Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania{Mkurabita}Dkt.Seraphia Mgembe amesema kuwa Wananchii waliopokea hati wanauwezo mkubwa wa Kuondokana na Umasikini kwa Kutumia hati zao kwa kushirikiana na wawekezaji mbalimbali watakaotaka kuwekeza hasa katika zao la korosho.

“Hii hati ni htai ambayo Vyombo vya fedha na Wawekezaji wanaamini kuwa wewe ndio mmiliki halali wa Shamba hilo kama kuna mtu anataka kuwekeza kwenye shamba lako na ili ajue kuwa wewe ndio mwenye shamba lazima umuoneshe Hati hiyo na katka wakati huu wa kilimo cha kisasa cha zao la Korosho,Wanaweza wakatokea watu wengi wakitaka kulima korosho Nachingwea na ili aweze kuingia ubia na wewe lazima umuoneshe Hati’’

Koini Mwanjisi ni Mkulima wa mazao ya Korosho na mahindi katika kijijji cha Mbondo Wilayani nachingwea tayari amepima Ardhi ya Heka saba na Kupatiwa hati anasema kwa sasa ameweza kufahamu jinsi ya kupata mikopo katika taasisi za kifedha ili kweza kulima kisasa zaidi.

“Sasa nimeoneshwa milango wapi nitaingilia kuweza kupata mkopo sababu nilikuwa nalima bila ya kuwa na nguvu za ziada lakini sasa hivi nimeshaoneshwa na Mkurabita nafikiri katika mika mingine inayokuja nitakuwa juu tofauti na hatua niliyonayo sasa hivi”alisema Mwanjisi.
mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Jason Reikiza akimkabidhi Hatimiliki za ardhi kwa Koini Mwanjisi katika hafla ya kukabidhi Hatimiliki za kimila miamoja {100} kwa wakulima wa kijiji cha Mbodo Wilaya ya Nachingewa mkoa wa Lindi.
Kutoka Kushoto Mratibu wa Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania{Mkurabita}Dkt.Seraphia Mgembe wakifurahi jambo na Mbunge wa iramba Mashariki Mwigulu Nchemba mara baada ya kupokea taarifa ya Mkoa Kuhusu Urasimishaji wa Ardhi katika Mkoa wa Lindi.
Naibu waziri Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa uma na Utawala Bora Marry Mwanjelwa wakijadili jambo na Mratibu wa Mkurabita Dkt.Seraphia Mgembe mara baada ya kumaliza kukagua Masjala ya Kijiji cha Mbondo kwa ajili ya kuhifadhi Hati za kimila za wananchi.
Naibu waziri Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa uma na Utawala Bora Marry Mwanjelwa akijadili jambo na wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa mara baada ya kumaliza kugawa hati miliki za kimila za Mashamba kwa wakulima wa Kijiji cha Mbondo kilichopo Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...