NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

KAMATI ya kudumu ya miundombinu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeielekeza wizara ya ujenzi kuwasilisha majibu ya msingi ya kimaandishi kuhusu matumizi ya fedha iliyowekezwa katika mradi wa mfumo wa anwani za makazi na postikodi. 

Aidha imeomba serikali iwekeze fedha ya kutosha kwenye mradi huo ambao utasaidia kutoa utambuzi katika maeneo husika na wageni kukuta miundombinu mizuri hasa ya mawasiliano. 

Akitoa maelekezo hayo, mwenyekiti wa kamati hiyo, Suleimani Kakoso wakati kamati ilipotembelea na kukagua miundombinu ya mfumo wa anwani za makazi na postikodi kata ya Tumbi, Kibaha mkoani Pwani, alisema ingefaa kuboreshwa katika raslimali fedha ili uweze kufanyiwa kazi haraka. 

Alifafanua, ripoti itakayowasilishwa na kueleza kinaga ubaga kuhusu mapato na matumizi itairahisishia kamati kujua changamoto zilizopo na wapi waongeze msukumo kwa lengo la kufanikisha utekelezaji wa mradi. 


Pamoja na hayo, Kakoso ameitaka jamii ilinde miundombinu iliyopo katika miradi mbalimbali inayowekezwa na serikali kwani nguzo moja inayojengwa katika mradi huo inagharimu sh. 156,000 gharama ambayo ni kubwa.

Nae naibu waziri wa ujenzi ,uchukuzi na mawasiliano, Elias Kuandikwa alisema, mradi utarahisisha ukusanyaji wa mapato kutoka vyanzo mbalimbali nchini.

Kuandikwa alielezea, mfumo huo wa anwani za makazi utaiwezesha Serikali kuwahudumia wananchi wake kirahisi ikiwa ni pamoja na kutoa ulinzi, kurahisisha mawasiliano miongoni mwa wananchi na Serikali.

Naibu katibu mkuu, wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano (MAWASILIANO) dkt. Jim Yonazi aliongeza kuwa ,katika nchi nyingi za viwanda na nchi zilizoendelea suala la miundombinu ikiwemo mfumo huo ni muhimu na linaeleweka kwa kila mtu katika kuanzisha, kukuza na kuendeleza uchumi wa viwanda.

Alisema, mfumo una mahitaji makuu matatu ikiwemo nguzo zilizosimikwa kwenye barabara zenye majina, vibao vilivyobandikwa kwenye nyumba /jengo na postikadi limekamilika kila kata/wadi inapostikadi yake.

"Unaweza kupata postikadi ya kata yoyote kupitia simu yako ya mkononi kwa kupiga *152*00#chagua 3 (ajira na utambuzi)"alifafanua dkt. Yonazi. 

Mkandarasi na mkuu wa chuo cha ufundi (VETA) Dodoma ,Ramadhani Mataka alisema wanaendelea na kazi vizuri na faida wanayoitoa ni ajira pamoja na kulipa kodi serikali na walishatoa mil 2.8 kulipa kodi. 

Kwa upande wake, msimamizi wa mradiambae pia ni mhandisi mkurugenzi wa huduma ya mawasiliano wizara ya ujenzi, Clarence Ichwekeleza, anasema wametekeleza mradi katika kata 112.

Alieleza wamepokea bilioni mbili ambapo bilioni 1.2 awamu ya kwanza na awamu ya pili sh. milioni 727.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...