Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (wapili kulia) akitoa maelekezo kwa uongozi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kuweka alama za mipaka madhubuti badala ya Mawe katika mipaka ya maeneo ya Chuo hicho, alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho kilichopo Jijini Mwanza jana kwa lengo la kutambua mipaka ya Chuo hicho pamoja na kuzungumza na wafanyakazi na wanafunzi wa Chuo hicho,wakwanza kulia ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya BW.Richard Mganga.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (wapili kushoto) akifanya ziara ya kukagua mazingira ya hostel za wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho kilichopo Jijini Mwanza jana,watatu kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Mganga na watatu kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Orest Mushi.Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (wapili kulia) akiwa anatoka kukagua mazingira ya choo katika moja ya hosteli za Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho kilichopo Jijini Mwanza jana, anayeongoza kutoka ni Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Mganga.


Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (wakwanza kulia) akikagua mipaka ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo Jijini Mwanza alipofanya ziara ya kikazi Chuoni hapo jana, katikati ni Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Mganga.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (katikati) akizungumza na wafanyakazi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo jijini Mwanza (hawapo pichani) jana alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho,wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Mganga,na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Orest Mushi.
Mhasibu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Bw.Mustapha Majura akimwomba Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (hayupo pichani) kupatiwa nafasi ya kusoma kozi fupi kwa mwaka ujao wa fedha za masuala ya uhasibu kufuatia mifumo utendaji wa kazi za uhasibu sasa kubadilika na kuwa za kieletroniki wakati wa kikao cha Wafanyakazi wa chuo hicho na Katibu Mkuu huyo jana alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (aliyeketi wapili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo Jijini Mwanza mara baada ya kumaliza kikao na Wafanyakazi hao jana alipofanya ziara ya kikazi katika Chuo hicho kilichopo jijini Mwanza,aliyeketi( wa tatu kushoto ) ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Bw.Richard Mganga na (wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw.Orest Mushi kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya alipofanya ziara ya kikazi katika Chuo hicho kilichopo Jijini Mwanza jana.

……………………………

Anitha Jonas – WHUSM ,Mwanza

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ameutaka uongozi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kupanda miti ya mbao kwa maeneo ya wazi ya chuo hicho badala ya kuacha ardhi hiyo bila matumizi rasmi.

Katibu Mkuu Mlawi ametoa agizo hilo jana alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho kilichopo Mkoani Mwanza kwa lengo la kuzungumza na uongozi na wafanyakazi wa chuo hicho mambo mbalimbali ikiwemo kuweka mikakati ya kuboresha chuo hicho pamoja na kujua mipaka ya chuo hicho.

“Chuo hichi kina eneo kubwa sana ekari 161 ni nyingi na eneo hili lote haliwezi kuendelezwa sasa hivi hivyo ni vyema mkapanda miti ya mbao itakayo wasaidia kuongeza kipato cha chuo na kupata rasilimali fedha itakayo wasaidia kufanya maendeleo katika chuo hichi wasalianeni na Wakala wa Misitu Tanzania watawashauri aina ya miti inayofaa kwa ardhi hii,”alisema Bibi.Mlawi.

Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Katibu Mkuu huyo ameusistiza uongozi wa Chuo hicho kufanya vikao na wafanyakazi wake pamoja na wanafunzi wa chuo hicho mara kwa mara ilikuweza kusikiliza kero zao na kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali,pia amewasihi watumishi hao kuzingatia maadili ya utumishi wa umma pamoja na kuwa na nidhamu kazini.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo Richard Mganga hicho alieleza kuwa Chuo hicho kimekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo madai mbalimbali ya watumishi ,uhitaji wa kuchimba kisima cha maji ilikuweza kuwa na maji ya kutosha kufuatia ongezeko la wanafunzi wa Chuo hicho.

“Udahili wa Wanafunzi kwa Mwaka huu umeongezeka na kufikia 261 na hivyo kulingana na miundo mbinu tuliyokuwa nayo awali kuwa na uwezo mdogo tumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji ya kutosha,hivyo tunaomba tusaidiwe kupata fedha za kuchimba kisima cha maji mapema ili kuondokana na kero hii,”alisema Mganga.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Chuo alitoa wito kwa watu kujitokeza kujakusoma Kozi mbalimbali za Michezo kwani Chuo hicho kinafundisha Diploma ya Uongozi na Utawala katika Michezo,Diploma ya Elimu ya Michezo pamoja na Diploma ya Ufundishaji Michezo

Pamoja na hayo nae Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Orest Mushi aliwatoa hofu watumishi wa Chuo hicho waliyokuwa na madeni ya malipo ya stahili mbalimbali kuwa hivi karibuni malipo hayo ya madeni yatafanyika kwa hazina wanatoa fedha hizo.

Vilevile nae Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Steven Dalasia aliusistiza uongozi huo kuandaa mpango wa manunuzi kwa bajeti ya 2019/2020 ili kupunguza hoja wakati wa ukaguzi wa mahesabu.

Halikadahali nae Mkufunzi wa Chuo hicho Bw.Omari Mataka aliupongeza uongozi wa wizara kwa kufanya ziara chuo hapo pamoja na kuwasililiza kero zao na kutoa majibu ya hoja zao mbalimbali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...