Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Mhe. Richard Kwitega akizungumza jambo na Wananchi na Wanafuzi kutoka shule mbalimbali ikiwemo Shule ya Msingi Meru ya wanafunzi wenye usikivu hafifu katika viwanja vya Shule ya Msingi Meru Mkoani humo katika matembezi ya Uhamasishaji wa Umma kuhusu umuhimu wa Afya ya Kinywa na Meno yaliyoanzia katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo , ambapo kilele itakuwa Machi 20, 2019, Mgeni Rasmi ni Waziri wa (TAMISEMI) Suleiman Jaffo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) 


NA KHAMISI MUSSA

Ambapo Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Mhe. Richard Kwitega "alisema"

Awali ya yote nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kushiriki kwenye matembezi haya yenye umbali wa kilometa 2.5 yaliyoanzia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuishia katika viunga vya uwanja wa shule ya msingi Meru.

Kwaupande mwingine niwashukuru pia waandaaji wa shughuli hii ya tukio hili lenye uhai mzima wa tasnia ya afya ya kinywa na meno, asanteni sana.

Aidha, nitumie nafasi hii kwakuwapongezeni nyote mlioshiriki kwenye matembezi yaha asubuhi hii, Ninawashukuru sana kwa kujumuika nasi katika shughuli hii muhimu yenye lengo la kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa afya ya kinywa na meno Tanzania.

Ndugu wananchi, Ninapenda kuchukua nafasi hii kuwaarifu kuwa matembezi haya yaliyoratibiwa na Chama cha Wataalamu wa Afya ya Kinywa na MenoTanzania (TDA) yanayofanyika kila mwaka kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya afya ya kinywa na meno Duniani.

Kama ilivyo kwa sherehe mbalimbali za maadhimisho, Sherehe hizi huambatana na kauli mbiu na kauli mbiu ya mwaka huu ni "SEMA AHH: CHUKUA HATUA ZINAZOZINGATIA AFYA YA KINYWA NA MENO" Kauli mbiu hii ni mwendelezo wa kampeni ya kipindi cha miaka mitatu zilizoanzishwa mwaka jana 2018 na Shirikisho la Vyama vya Afya ya Kinywa na Meno Duniani chini ya kibwagizo cha kauli mbiu kisemacho "Sema Ahh", kwa mwaka jana 2018 kauli mbiu ilikuwa "Sema Ahh; Fikiri Kinywa Fikiri Afya"ikilenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu mahusiano ya afya ya kinywa na afya ya mwilikwa ujumla.
Madaktari na Wanafunzi wakiwa katika maandamano hayo 

Rais Mwandamizi wa Chama cha Wataalamu wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania, Dkt. Deogratias Kisala akizungumza jambo wakati wakati wa matembezi ya Uhamasishaji wa Umma kuhusu umuhimu wa Afya ya Kinywa na Meno yaliyoanzia katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo , ambapo kilele itakuwa Machi 20, 2019, Mgeni Rasmi ni Waziri wa (TAMISEMI) Suleiman Jaffo.


Kwa upande wa Rais Mwandamizi wa Chama cha Wataalamu wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania, Dkt. Deogratias Kisala "alisema" Magonjwa ya fizi na kutoboka kwa meno ni maradhi ambayo huwapata watu wengi sana ulimwenguni.

Tafiti zilizofanywa na shirikisho la afya ya kinywa na meno duniani zinaonyesha kwamba tatizo la kutoboka kwa meno ndio linaathiri watu wengi Duniani. Aidha, nchini mwetu, inaripotiwa kuwa kati ya watu 10 wenye umri wa miaka 45 na zaidi, watu 8 wanakabiliwa na matatizo ya ugonjwa wa fizi. 

Magonjwa ya kinywa na meno yanaweza kuzuilika kwa kufuata njia sahihi za usafishaji wa kinywa, kusafisha meno mara mbili kwa kutwa, kutumia dawa ya meno yenye madini ya floridi na kumuona daktari wa meno angalau mara moja kwa mwaka Kinga ni bora kuliko tiba na gharama za matibabu ni kubwa kuliko gharama za kinga

Tunatumaini wananchi wamepokea jumbe mbalimbali zilizokuwa kwenye mabango wakati wa matembezi yetu ya leo, Chama cha wataalamu wa afya ya kinywa na meno tukishirikiana na Serikali na wadau wetu tumeratibu shughuli mbalimbali za uhamasishaji wa afya ya kinywa na meno nchini kote.

Toka tarehe 14 Machi shughuli za kutoa elimu, uchunguzi wa afya ya kinywa na meno na matibabu bila malipo kwa nananchi yanayoendelea kutolewa katika mikoa mbalimbali nchini. Kitaifa, maadhimisho yanafanyikia mkoani hapa, katika mkoa wa Arusha na tutatoa huduma katika shule za watoto wenye mahitaji maalumu za Meru, Uhuru, Makumbuso, Shangarawe na pia tutatoa huduma kwa wananchi katika kituo cha Afya cha Themi ifikapo Kilele cha maadhimisho hayo ni siku ya tarehe 20, Machi.

Tunategemea kuwa tumetoa huduma kwa watu takribani 4000 hapa mkoani Arusha na wananchi zaidi ya elfu arobaini na saba (47000) nchini kote
Ndugu mgeni rasmi, Mwaka jana maadhimisho kama haya tulitoa huduma za elimu ya afya, ushauri na matibabu kwa zaidi ya watu elfu thelathini na nane (38000) nchini kote.

Hii ilipelekea chama chetu kupewa tuzo ya kimataifa inayojulikana kama "Most Educative Award" inayotolewa na Sirikisho la Vyama vya Afya ya Kinywa na Meno Duniani (FDI), Zawadi hii imeliletea heshima kubwa sana nchi yetu.Napenda kutoa shukurani za dhati kwa serikali yetu kwa ushirikiano mkubwa inayo tupa katika kuboresha huduma ya afya ya kinywa na meno nchini.

Aidha tunaipongeza serikali kwa kupitisha na kuufanyia kazi muswada wa sheria ya madaktari, madaktari wa meno na wataalamu wa Afya shirikishi ya mwaka 2017 tunatumaini sheria hiiitasaidia kuboresha huduma za Afya kwa jamii na kuongeza ufanisi na tija kwa wataalamu wa Afya 
Mtunza hazina wa Chama cha Wa Afya ya Kinyewa na Meno Tanzania, Dkt. Arnold Mtenga (kulia) kishiriki maandamano hayo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...