Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
UONGOZI wa Klabu ya Simba umetangaza viingilio vya mchezo wao wa mwisho wa kundi D wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika utakaopigwa Mach 16 katika Uwanja wa Taifa.

Mchezo huo wa mwisho kati ya Simba na As Vita utachezwa kuanzia majira ya saa 1 usiku ambapo mechi zote za kundi hilo zitachezwa ndani ya muda mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Ofisa habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa mchezo huo utakuwa katika viingilio vitatu na kiingilio cha chini kitauwa ni shilingi 3000 kwa mzunguko na Orange.

Manara amesema, kwa upande wa VIP B kiingilio kitakuwa ni  10,000 na VIP A ikiwa 20,000 huku Platnums itakuwa ni 100,000.

Amesema kuwa, mechi hiyo itachezwa muda mmoja na Al Ahly dhidi Js Saoura ukiwa ni mchezo wa mwisho wa kundi hilo ili kuweza kupata timu mbili zitakazokwenda hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

"Tiketi ya Platnums itampa usafiri shabiki kwenda Uwanjani akitokea Serena Hotel mpaka Uwanjani na atakaa sehemu ambayo itaambatana na vinywaji huku akipewa na jezi,"amesema Manara.


Manara amewaomba mashabii kujitokeza kwa wingi katia mchezo huo ili kuweza kuujaza Uwanja huo ikiwa ni moja ya hamasa kwa timu wawapo Uwanjani. Ameeleza kuwa timu yao ndiyo namba moja Afrika kwa kuweza kujaza Uwanja unaoingia takribani watu 60,000.

Simba inaingia kwenye mchezo huo wakiwa na  kumbukumbu mbaya ya kufungwa goli 5-0 kwenye mchezo wao wa awali uliofanyika nchini DR Congo na pia kutoka kupoteza  2-0 dhidi ya JS Saoura katika mchezo wa mwisho uliopigwa huko Bechar, Algeria mwishoni mwa wiki hii.


Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na wadau wa mpira hapa nchini, itapigwa majira ya saa 1 za usiku katika Uwanja wa Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...