WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (kushoto), akisoma moja ya bango liloandikwa na wananachi kabla ya kuanza mkutano wake wa hadhara na wananchi wa Tarafa ya Kimamba, Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro, alipofika katika tarafa hiyo kwa lengo ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo inaleta uvunjifu wa amani katika eneo hilo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Adamu Mgoyi. Lugola alisema chanzo ya migogoro ya ardhi Wilayani humo ni kutokana na kuibuka wanasheria feki ambao wanawarubuni wananchi kushindwa kufauata sheria za nchi.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, akizungumza na mamia ya wananchi wa Tarafa ya Kimamba, Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro, alipofika katika tarafa hiyo kwa lengo ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo inaleta uvunjifu wa amani katika eneo hilo. Lugola alisema chanzo ya migogoro ya ardhi Wilayani humo ni kutokana na kuibuka wanasheria feki ambao wanawarubuni wananchi kushindwa kufauata sheria za nchi.
 WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza mwakilishi wa wananchi katika Tarafa ya Kimamba, Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro, akisoma hukumu zilizotolewa na mahakama kuu na ya rufaa ambayo inaonyesha Mfuaji Lipasio Mbokoso (hayupo pichani) wa Tarafa hiyo alishinda kesi hiyo dhidi ya wananchi wachache waliofungua kesi ya ardhi wakidai ni mali yao. Lugola alisema chanzo ya migogoro ya ardhi Wilayani humo ni kutokana na kuibuka wanasheria feki ambao wanawarubuni wananchi kushindwa kufauata sheria za nchi Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Mkazi wa Tarafa ya Kimamba, Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro, Iris Diamond, akitoa kero yake kuhusiana na mgogoro wa ardhi kati yake na wananchi wa Tarafa hiyo. Lugola alisema chanzo ya migogoro ya ardhi Wilayani humo ni kutokana na kuibuka wanasheria feki ambao wanawarubuni wananchi kushindwa kufauata sheria za nchi  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Na Felix Mwagara, Kilosa

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ametumia saa tano kuwatuliza wananchi wa Tarafa ya Kimamba Wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro, ambao walikuwa na hasira kali wakilalamika kunyang’anywa ardhi na wafugaji pamoja na Polisi kuwanyanyasa wananchi hao kwa kuwaweka ndani.

Waziri Lugola ambaye aliwasili saa sita mchana akitokea mjini Morogoro kwa ajili ya kutekeleza ahadi yake kwa wananchi hao baada ya kuwaahidi wiki iliyopita alipofanya ziara katika Tarafa hiyo ambayo ina wakazi zaidi ya elfu hamsini, ili aweze kutatua kero zao za ardhi wakiwa na nyaraka zao za uthibitisho.

Kabla ya mkutano wa hadhara na wananchi hao, Waziri huyo alifanya kikao cha ndani na viongozi wa Wilaya hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya, kwa lengo viongozi hao kumpa sura halisi ya mgogoro huo ambao unaelekea katika uvunjifu wa amani.

Lugola aliwasili eneo la mkutano mara baada ya kumaliza kikao cha ndani, ambapo alipokelewa na mabango ya wananchi ambayo yalikuwa yameandikwa ujumbe mbalimbali ikiwemo ‘Polisi wa Dumila wanatumika kuwanyanyasa wananchi na polisi wa Chanzulu wanakamata watu na kuwaweka ndani wananchi wanaotafuta haki ya ardhi’, wafugaji wanapora ardhi zetu, polisi wanapewa rushwa na wafugaji kutuweka ndani’. 

Akizungumza na mamia ya wananchi hao, Lugola alisema amekuja kusikiliza kero za wananchi hao baada ya kutoa ahadi yake wiki iliyopita, hivyo anatumaini wananchi hao wanavielelezo kama alivyowaagiza waje nazo katika mkutano huo.

Lugola alisema Jeshi la Polisi alihusiki na masuala ya ardhi isipokuwa limekua likichukua hatua pale migogoro hiyo inapopelekea kwenye uhalifu ama uvunjifu wa amani.

Lugola alishangiliwa na wananchi hao alipowaita waje mbele ya meza kuu ili waweze kutoa kero zao, ndipo idadi kubwa ya wananchi hao waliitikia wito huku baadhi yao wakiwa na nyaraka mbalimbali kama walivyoelekezwa na Waziri huyo waje nazo katika mkutano huo.

Licha ya wananchi hao kutoa kero mbalimbali lakini tatizo kubwa walikuwa wanamtuhumu mfugaji maarufu ambaye ni Mmasai katika Wilaya hiyo, Lipasio Mbokoso, anayedaiwa kunyang’anya ardhi zaidi ekari 270 ambazo wanadai sio zake lakini anatumia nguvu ya fedha kuichukua ardhi ya wananchi hao.

Waziri Lugola alimwita Mbokoso katika mkutano huo ili aweze kujitetea kwa nyaraka zake, ndipo ikajulikana kuwa Mmasai huyo ardhi hiyo ni mali yake halali baada ya kushinda kesi iliyofunguliwa na wananchi hao mahakamani. 

“Nyaraka zinaonyesha Mbokoso ni mmiliki halali wa ardhi hii, na pia wananchi ambao nimewataja walifungua kesi, na Mbokoso akashinda kesi hiyo mahakama kuu, baadaye mkakata rufaa mkaenda mahakama ya rufaa, pia akashinda, ndugu wananchi naomba mueleze na hakuna haja ya malumbano, huyu ni mmiliki halali wa mali hiyo, musidanganywe na mtu yeyote, fuateni sheria pamoja na kuiheshimu hukumu ya mahakama,” alisema Lugola.

Aliongeza kuwa, kuna baadhi ya wanasheria feki katika eneo hilo wanawarubuni wananchi kwa kuwapotosha na kuwasababisha munaingia katika migogoro ya ardhi na amani inatoweka katika eneo hilo kwasababu tu ya watu wachache ambao wanawapotosha. 

“Wanasheria feki ndio wanaochangia migogoro ya ardhi katika sehemu mbalimbali ya Wilaya ya Kilosa, nawataka wananchi kutowatumia badala yake mufuate sheria kama inavyoelekeza,” alisema Lugola.

Kutokana na matatizo ya ardhi kuendelea kutokea katika eneo hilo, Waziri Lugola amemtaka Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Wilbroad Mutafungwa kuchunguza nyaraka zote za migogoro ya ardhi inayowasilishwa na wananchi ili kujua kama ni halali au zimeghushiwa.

Sambamba na hilo, Lugola amemtaka Kamanda huyo kuwachukulia hatua kali za kinidhamu askari wote wasiokuwa waadilifu katika eneo hilo na Mkoa kwa jumla, watakaohusika kuwanyanyasa wananchi hasa katika masuala ya ardhi. 

Kauli ya Waziri huyo ilileta furaha kwa sehemu kubwa ya wananchi hao licha ya kuwa baadhi yao wakilalamika kuwa, Polisi wameshindwa kutatua kero zao na kuwadharau wakulikuma na kuwathamini wafugaji, hata hivyo Waziri huyo aliahidi kufuatilia mara kwa mara amani ya eneo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...