Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya ndege ya Air Tanzania aina ya Airbus A220-300 wakati akielekea nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa Africa Now Summit 2019 unaoanza kesho tarehe 12 mjini Kampala Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Uganda na kupokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Philemon Mateke pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt. Aziz P. Mlima katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebe.
Makamu wa Rais pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaru wamesafiri na ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la Tanzania aina ya Airbus A220-300 (Dodoma) kutoka jijini Dar es Salaam mpaka Entebe kupitia Kilimanjaro.

Kesho Makamu wa Rais atashiriki mkutano wa mwaka 2019 wa “Africa Now Summit 2019” ambao utafunguliwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambapo viongozi mbalimbali wa Afrika wanakutana ili kupata majibu ya changamoto za Afrika katika masuala ya kiuchumi.

Katika mkutano huo wa Viongozi wa Afrika, Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambapo katika mada mbalimbali zitakazojadiliwa Makamu wa Rais atazungumzia suala la Uongozi unaohitajika kuchochea mabadiliko ya Kijamii na Uchumi Afrika. 

Viongozi wengine watakaotoa mada ni Rais wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (UA) Mhe. Abdel Fattah el Sisi; Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa; Makamu wa Rais wa Kenya Mhe. William Ruto; na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Ahmed Abiy na Rais Paul Kagame wa Rwanda. Mada zote hizi zitajikita kwenye kuonesha chachu ya Uongozi katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika. 

Mkutano utamalizika tarehe 13 Machi 2019 utaanza na hotuba kutoka kwa Rais wa Somalia Mhe. Mohamed Abdullahi na baadae kufungwa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.

Makamu wa Rais ataambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Dkt. Aziz P. Mlima mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe nchini Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Mhe. Philemon Mateke mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe tayari kwa kushiriki mkutano wa Africa Now Summit 2019 utakaofanyika mjini Kampala tarehe 12 na 13 mwezi Machi, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Dkt. Aziz P. Mlima (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebe, wengine pichani ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Mhe. Philemon Mateke (kushoto).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...