Na Sultani Kipingo
Aghalabu ndege inapopata dharura angani, waongoza ndege waliopo ardhini hawasiti kuiruhusu kurudi uwanjani, wakati mwingine kutokana na kusahaulika kitu. Majuzi kati katika uwanja wa Mflamu Abdulazizi wa Saudi Arabia mama mmoja alisahau motto wake mchanga hapo uwanjani.

Yaani huyo mama, aliyekuwa anasafiri na ndege ya Shirika la Ndege la Saudi Arabia, alisahau kichanga chake kwenye eneo la kusubiria la wanaoondoka. Kwa mujibu wa gazeti la Gulf News, japokuwa yeye ni mzazi, mama huyo alipanda hiyo ndege akiwa hana shaka na jambo lolote.

Ni wakati ndege ikiwa imeshapaa angani ndipo akakumbuka kwamba kaacha kichanga uwanjani! Na mara tu baada ya kugundua hilo, akawaarifu wahudumu wa ndege kwamba kasahau motto mchanga uwanjani, na kumfanya rubani wa Ndege namba SV832 kutoka mji mkuu wa Saudi Arabi, Jeddah, ikielekea Kuala Lumpur, Malaysia, irudi uwanjani.

Tukio hilo lilishangaza kila mtu wakiwemo wahudumu wa ndege, abiria wenzake na hata waongoza ndege uwanjani Jeddah. Video inayoonesha rubani wa ndege hiyo akiomba ruhusa kurudi uwanjani kumchukua motto mchanga aliyesahaulika imeshika kazi mitandaoni huku wengi wakijiuliza mtu unasahau vipi motto wako?

“Ndege hii inaomba ruhusa kurudi…kuna abiria kasahau kichanga chake uwanjani, maskini”, rubani anasikika katika video hiyo.

Waongoza ndege walichukua dakika kadhaa kufikiria itifaki ipi itumike katika kuruhusu ndege kurejea uwanjani kwa sababu kama hiyo.
“Haya rudi tena getini. Hili ni jambo jipya kwetu!” anasema mmoja wa waongoza ndege. Hata hivyo ndege ikatua na mama akaungana na kichanga chake na kuendelea na safari baadaye.

 The ATC executives spent several minutes figuring out the protocol to be observed during such incidents. “Ok, head back to the gate. This is totally a new one for us!” says one of the ATC operator. The woman was finally reunited with her baby at the airport. 
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...