Na Woinde Shiza-Arusha

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi  Stella Manyanya amewataka wawekezaji waliobinafsihiwa baadhi ya viwanda kutumia viwanda hivyo kwa lengo husika na sio kuvitumia kwa matumizi mengine ambayo haya kukusudiwa .

Naibu Waziri aliyasema hayo jana  wakati wa ziara ya kamati ya kudumu ya Bunge viwanda ,biashara na Mazingira ilipotembelea katika kiwanda cha bia cha kampuni ya TBL Arusha na kujionea jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi

Alisema kuwa Serikali haita mfumbia macho mwekezaji yeyote aliyebinafsishiwa kiwanda na badala ya kukiendeleza ,akakigeuza kufanyia shughuli nyingine tofauti na ile iliyo kusudiwa .

"wale ambao wamepewa viwanda kwa nia ya kuviendeleza na hawajafanya hivyo wamefanya vitu vingine, serikali haitaona hatari ya kuvipokonya viwanda hivyo kwa wawekezaji ambao walibinafsishiwa΄΄alisema Naibu Waziri

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge viwanda ,biashra na mazingira Suleiman Saddiq aliipongeza Tbl kwa kazi wanayofanya na jinsi wanavyolipa kodi kwa serikali pia aliwahaidi kupeleka bungeni baadhi ya changamoto ambazo wamezisema ikiwemo la kuongezewa eneo la kiwanda pamoja na kupunguziwa ushuru wa mabango .

Aidha pia kamati hiyo ilipotembelea katika kiwanda cha Camatec ilitaka serikali ifanye kila iwezekanavyo kuweka fedha za maendeleo nyingi ili vitu vinavyotengenezwa na camatec viwe na ubora zaidi na pia ijitaidi kupeleka fedha za bajeti ambazo zimepangwa kwenye kiwanda hicho kwaa wakati ili kiweze kufanya kazi jinsi ipasavyo na wananchi

Aidha Kamati hiyo ya bunge imeishauri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuviunganisha viwanda vya Cametec,Temdo na SIDO kwani viwanda hivi vina tegemeana na pia ndio nguzo pekee kuelekea uchumi wa Viwanda, hivyo ni lazima kusaidiwa kupata teknolojia za kisasa ili kusaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora na zenye ushindani katika masoko 
Pichani kushoto ni Mpishi wa bia kampuni ya TBL Richard Mkojera akitoa maelezo kwa  Naibu waziri wa viwanda ,biashara na uwekezaji Mhandisi  Stella Manyanya  namna bia zinavyotengenezwa kiwandani hapo.
Pichani ni Naibu Waziri wa viwanda ,biashara na uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya akitazama namna bia zinavyowekwa lebo kiwandani hapo
Mkurugenzi wa Masoko kanda ya kaskazini James Bokela akimuelekeza Naibu waziri namna mashine ya TRA inavyohesabu beer zinavyo zalishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...