Na Moshy Kiyungi,Tabora.

Mariah Carey alizaliwa toka kwenye familia yenye asili mataifa tofauti, ilibaguliwa na kufanyiwa fujo kila mara.

Familia hiyo ilijikuta ikisulubiwa kwa kuchomewa na kutupiwa vitu nje ya nyumba yao, mbwa wao wakinyweshwa sumu na risasi zikipigwa dirishani kwao.

Mariah Carey ni nani?

Ni mwanamuziki aliyezalizwa Machi 27, 1970 katika kitongoji cha Huntington jijini New York, nchini Marekani.

Baada ya kuzaliwa alipewa majina ya Mariah Angela Carey. Ni mwanamuziki mwenye mafaniko makubwa anayejulikana kila pembe za dunia.

Makuzi ya Mariah ni ya kuhuzunisha kwa jinsi alivyopitia msoto, maisha ya dhiki, msongo wa mawazo na kutengwa na jamii.

Mama yake Mariah ni Patricia Hickey, Mmarekani mwenye asili ya Ireland na baba yake Alfred Roy ni Mmarekani mweusi mwenye asili ya Venezuela,.

Mariah akiwa na umri wa miaka 16, aliingia shule Kati ya Oldfield. Huko ndiko akagundua kuwa nacho kipaji kingine cha kuandika nyimbo zake.

Lakini akaanza kutoroka na kukwepa masomo akibakia ghetto kuandika nyimbo, kwani tayari alishaingiza akilini mwake ndoto za kuwa mwanamuziki maarufu.

Alipoingia Harborfield High School, alianza kusafiri kwenda Manhattan na kurudi ili kusoma muziki na wataalamu waliobobea.

Baadaye Carey ilibidi alale akiwa mchovu sana, kwa kuwa alilazimika kuanza kusaka fedha kuingia studio kwa kufanya kazi za ziada baada ya ya masomo,. Pia alitakiwa kupata fedha za kulipia nyumba ndogo ya kupanga waliokuwa wakiisihi na mama yake.

Carey alilazimika kufanya kazi za kuosha nywele za watu saluni, pia alifanya kazi ya kuhudumia kwenye migahawa ili kupata fedha.

Mwaka 1987, alianza masomo yake Harborfields High School na kwenda Manhatan ambako rasmi alianza kurokodi nyimbo na baada ya mwaka mmoja akaanza kuona matunda ya kazi zake.

Novemba mwaka huohuo, Carey alikutana na kigogo wa muziki Mattola ambaye aliingia naye mkataba wa kurekodi albamu. Hapo ndipo alipotoa albamu yake ya kwanza iitwayo “Mariah Carey” mwaka 1990 wakati huo akiwa na umri wa miaka 20.

Albamu hiyo ilikuwa na mafanikio makubwa ikiwa na nyimbo zilizokaa kwa muda mrefu No. 1 kwenye chati kwa nyakati tofauti ambazo ni “Vision of Love”, “Someday”, “Love takes Time” na “I Don’t Want to Cry”.

Carey aliyetamba na nyimbo kama Touch my Body, I Still Believe, We Belong Together, My All, Without You na Always Be My Baby. Nyimbo hizo zilimletea sifa kubwa diniani kote.

Ameuza zaidi ya albamu milioni 200 duniani kote . (Piga hesabu, hata kama albamu moja ni shilingi 1,000 maana yake ana bilioni 200).

Pamoja na mauzo hayo, Carey pia ‘alipiga’ pesa nyingi aliposaini mkataba na Virgin Records mwaka 2000 akitokea Columbia Records kwa bosi Motola ambapo alilamba dola milioni 100. (zaidi ya Sh. Bilioni 227 za Kitanzania)

Mariah Carey ana tuzo tano za Grammy, 19 za dunia, 10 za Marekani na 14 za Billboard.Hili ni somo tosha kuwa ukipambana bila kukata tama, mwisho wa siku ni lazima utaona matunda.

Au kwa mneno ya Kiswahili “Mvumilivu hula Mbivu”Hata hivyo kwa upande wa pili wa maisha yake, Carey amebadilisha wanaume wengi sana hadi kufikia umri huu wa miaka 50.

Alianza kutoka kimapenzi na bosi wake Mottola wakati akirekodi albamu ya kwanza, na walioana Juni 2005, 1993 lakini wakatengana Mei 30, 1997.

Tangu 1998 hadi 2001 alikuwa kwenye uhusiano na mwanamuziki Luis Miguel. Alikutana na muigizaji wa Nick Cannon wakati wa kushuti video yao ya wimbo wa “Bye Bye’’. Waakaza mahusiano ya kimapenzi na hatimaye wakaoana Aprili 30, 2008, na Aprili 30, 2011 walifanikiwa kupata watoto wawili mapacha Moroccan na Monroe, Cannon Agosti 2014 alithibitisha kutengana na Carey .

Aidha Carey alikutana na James Parker bilionea wa Australia , wakatangaza kuchumbiana.Hadi kufikia Oktoba walikuwa tayari wamekorofishana na kusitisha uchumba wao.

Carey ni Muanglicana. Mwaka 2006 alitamka kuwa “Naamini nimezaliwa mara ya pili. Nadhani nilichobadilika ni vipaumbele vyangu na uhusiano wangu na Mungu.Najisikia tofauti nisipokuwa na muda binafsi wa kusali. Mimi ni mpambanaji, lakini nimejifunza kuwa na maamuzi ya mwisho .

Chochote Mungu anachotaka kitokee ndicho kinatokea. Ni kwa Neema za Mungu bado nipo”.

Huyu ndiye Mariah Carey mweye Ukwasi lufufu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...