Na Said
Mwishehe,Globu ya jamii
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni ameonesha kukerwa na kitendo cha askari wa wawili wa Kikosi cha Usalama
Barabarani, ambao wameonekana kwenye video kupitia mitandao ya kijamii
wakimtukana dereva na kumpiga yeye na abiria wake huku akieleza kuwa tayari wamekamatwa na
kuwekwa ndani ili sheria ichukue mkondo wake.
Kukamatwa kwa askari hao kumetokana na agizo lililotolewa na
Mhandisi Masauni ambapo amesema katu Serikali haiko tayari kuona Jeshi la
Polisi likichafuliwa na baadhi ya askari waliokosa uadilifu.
Akizungumza leo ijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa
mafunzo ya uchoraji la usalama barabarani, Masauni amesema kumekuwa na
malalamiko mengi ya madereva kubambikiwa makosa au askari kufanya vitendo
vilivyo kinyume na mwenendo mwema wa jeshi la polisi.
“Kuna video ambayo tangu jana imeonekana ikisambaa kwenye
mitandao ya kijamii ikiwaonesha askari wakimtukana dereva pamoja na abiria
waliokuwamo na si hivyo tu ilifika hadi kumpiga. Baada ya tukio hili
nilimuagiza Kamanda wa Kiko cha Usalama Barabarani achukue hatua kwa suala
hili. Kwa taarifa ambazo ninazo tayari wamekamatwa,"amesema.
Amesema ikitokea
mtumiaji yoyote wa barabara amefanyiwa vitendo vyovyote asisite kuwasiliana na
uongozi wa askari aliyefanya vitendo hivyo.“Na ikitokezea uongozi wa askari
husika anatetea au kutochukua hatua muafaka, mlalamikaji apande kwa uongozi wa
juu na ikibidi afike hata kwangu nani mitachukua hatua stahiki na utapata
mrejesho.
Kuhusu suala la
usalama barabarani, Mhandisi Masauni amesema anaipongeza Kampuni ya Mafuta ya
Puma kwa kuendesha program hiyo ambapo pia alizitaka kampuni zingine kuiga
mfano huo kwa kuwekeza kwenye ulinzi na usalama wa watoto kwani ni Taifa leo
kesho na wateja wa kesho pia.
“Programu hizo
zimekuwa zikikabiliw na changamoto mbalimbali za kifedha. Ninaomba kutumia
fursa hii kuomba uongozi wa Puma kukisaidia Kikosi cha Usalama Barabarani
kuzifikia shule zote nchini kwa kupitia askati walioko kwenye maeneo yote
nchini.Namuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani kuanza mchakato wa
kuandaa andiko la kutoa mafunzo kwa shule zote nchini na kuliwasilisha kwenu
(Puma) ili muone namna yambavyo mnaweza kusaidia kuokoa kizazi chetu cha
kesho,” alisema Masauni
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...