Jeshi la Polisi nchini limeelekezwa kutumia wafungwa ili kuweza kuokoa kiasi cha Shilingi Milioni Mia Mbili  kati ya Milioni Mia Saba zilizotolewa na Rais Dk. John Magufuli   katika Mradi wa Ujenzi wa Mabweni na Madarasa ya  Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo  Kurasini jijini Dar es Salaam.

Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipotembelea majengo chakavu ya chuo hicho baada ya kupokea kiasi cha Shilingi Milioni Mia Saba alizoahidi Rais Dkt. John Magufuli akihutubia katika mahafali ya kuhitimisha Mafunzo ya Kozi za Uofisa na Ukaguzi Msaidizi  chuoni hapo mwishoni mwa mwaka jana

“Wizara ina taasisi ya magereza ambayo ina nguvu kazi ya kutosha, na Rais alishaagiza wafungwa watumike katika shughuli za uzalishaji, sioni sababu ya kutumia kiasi hicho cha pesa kuwalipa vibarua wa nje, naagiza muwasiliane na Jeshi la Magereza pamoja na kikosi cha ufundi kilichopo ndani ya Jeshi la Polisi ili muweze kuona ni vipi mnaokoa kiasi hicho”alisema Masauni

Akitoa taarifa ya awali ya ujenzi huo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi, Naibu Kamishna Anthony Rutashuburugukwa alitaja  majengo yatakayojengwa kuwa ni ghala la chuo, madarasa matatu,bweni moja la askari wa kiume na bweni lingine la askari wa kike.

Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina wanafunzi wa chuo hicho walimshukuru Rais Dkt. Johh  Magufuli kwa kiasi cha fedha alichotoa ili kuweza kujenga sehemu mbalimbali za chuo hicho ikiwemo mabweni ambayo wamekiri ni chakavu na si rafiki kwa matumizi ya binadamu.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza  na  Askari  Polisi  ambao  ni  wanafunzi  katika  Chuo cha Taaluma ya  Jeshi  la  Polisi, wakati  alipotembelea  chuoni  hapo  kufuatilia maandalizi  ya awali  baada  ya  jeshi  hilo  kupokea kiasi cha Shilingi Milioni Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho.Ziara hiyo imefanyika  leo jijini Dar es Salaam. Picha  na  Wizara  ya Mambo ya Ndani  ya Nchi
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitembelea maeneo ya Chuo cha Taaluma ya Polisi  ambacho hivi karibuni kimepokea Shilingi Milioni Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya chuo hicho, kulia ni Mkuu wa Chuo, Naibu  Kamishna, Anthony  Rutashuburugukwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akitembelea maeneo ya Chuo cha Taaluma ya Polisi  ambacho hivi karibuni kimepokea Shilingi Milioni Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli  kwa  ajili  ya  ujenzi  wa majengo ya chuo hicho,Wengine  ni  viongozi wa chuo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi wakati wa ziara katika  Chuo  cha Taaluma  ya  Polisi, jijini Dar es Salaam  ambacho hivi karibuni kimepokea Shilingi  Milioni  Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa  majengo  ya  chuo hicho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...