Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

BAADA ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa kuamua kurejea Chama Cha Mapinduzi(CCM), Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amesema kwa kuwa ameondoka basi akawe mkweli huko alikokwenda. 

Lowassa wakati wa kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 aliondoka CCM na kwenda Chadema ambapo wakati wa mapokezi yake Mbowe alisema amebadili gia angani. Hivi karibuni Lowassa alirejea CCM akisema amerudi nyumbani. 
Akizungumza leo Machi 16,2019 jijini Dar es Salaam Mbowe amesema kuwa waandishi wa habari wamekuwa wakimuuliza kuhusu msimamo wa Chadema baada ya Lowassa kuondoka. 

"Chama chochote cha siasa kina wajibu wa kujenga chama ikiwa pamoja na kuongeza wanachama na katika kuongeza huko wanachama tulimuongeza na mzee Lowasaa mwaka 2015.Nataka kulizungumza kwa kifupi sana, vyama vyetu vya siasa vinavuna watu mbalimbali, wapo wema, wapo wasio wema, wapo wanaopenda madaraka, wapo kila mmoja kwenye roho yake anajua anataka nini katika siasa, hapa mezani huenda tunaajenda tofauti. 

"Tutumie karama zetu kwa namna ambavyo Mungu ametujaalia kupinga uovu , kulaani yasiyo ya haki, kupigania haki na usawa.Ukiona kuna mambo mengi yanatokea halafu mtu yuko kimya ni bora akishindwa kuwa na sisi basi usiwe na sisi.Mheshimiwa Lowassa nilisikitika kwasababu tulimpokea kwa nia njema sana,"amesema. 

Ameongeza kwa kuwa ameondoka na kwenda CCM basi akiwa huko kwenye Chama chake kipya awe mkweli kwa kuwaambia yale yanayoonekana hayako sawa huku akifafanua Chadema haiko tayari kuona damu inamwagika kwa sababu ya kutafuta madaraka. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...