HALMASHAURI ya jiji la Dar es salaam imesema kuwa imepanga kuomba zabuni ya utoaji huduma ya usafirishaji abiria kupitia mabasi yaendayo haraka kutoka Kariakoo Gerezani hadi Mbagala.

Kauli hiyo imetolewa jijini hapa leo na Mstahiki Meya Isaya Mwita mara baada ya kumalizika kwa kikoa cha baraza la madiwani lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee.

Meya Mwita amesema kuwa tayari Wakala wa mabasi yaendayo haraka wameshatangaza zabuni ya ujenzi wa awamu ya pili ya miundombinu ya mabasi itakayoanzia Kegerezani hadi Mbagala hivyo kama jiji limeona kunahaja ya kuomba zabuni hiyo ilikutoa huduma hiyo ya usafiri.

Amefafanua kuwa jiji linania ya kuomba zabuni hiyo kutokana na kuwa wanaweza kutoa huduma hiyo ili kusaidia adha ya foleni iliyopo kwa sasa katika maeneo ya Mbagala.

“ Tunatarajia kuomba zabuni ya kutoa huduma ya kusafirisha abiria hapa jijini ,iwapo tutakubaliwa basi kama jiji nalo litakuwa miongoni mwa watoa huduma hiyo” amesema Meya Mwita.

Tunajua kwamba pesa tunazo, nauwezo wakutoa huduma hiyo tunao,kwahiyo wakazi wa jijini hapa wafahamu kuwa kama tutakubaliwa tutatoa huduma hiyo, ndio mana leo nimewaeleza madiwani kwamba uliangalie jambo hili kwa umuhimu wake ilitujiandae” ameongeza.

Katika hatua nyingine baraza hilo limepitisha kwa kauli moja taarifa mbalimbali za utendaji na miradi mbalimbali zilizotolewa na wenyeviti wa kamati mbalimbalimbali za jiji.

Imetolewa leo Machi 12 na Christina Mwagala .Afisa habari ofisi ya meya wa jiji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...