Na Khadija Seif, Globu ya jamii
MCHEKESHAJI
chipukizi visiwani Zanzibar, Abdulnadhif Shaka Hassan ‘Dullyzo’,
ametoa ujumbe kwa vijana ambao wanataka mafanikio ya haraka.
Akizungumza
leo Dullyzo amesema umaarufu na mafanikio alioyapata hayakuja kimiujiza
kwani aliamini ndoto zake pamoja na kujishugulisha na kazi mbalimbali
za kijamii.
"Kabla sijawa
mchekeshaji nilikua nacheza ngoma na ndio kilikuwa kipaji changu
ambacho kilikua kinaniingiza fedha za kujikimu kiuchumi na kuendesha
familia," amesema
Hata
hivyo ameeleza nini kilimvutia na kuingia kwenye tasnia ya vicheko huku
akimtaja Dullivan kama mtu anayefata nyayo zake katika kazi.
“Wakati
naanza kumuiga Dullvani, nilitamani siku nikutane naye ili anifundishe
baadhi ya njia anazotumia na nashukuru Mungu tumeweza kuonana katika
tamasha lililofanyika siku chache zilizopita lililoandaliwa na
Zanzibarglamr la mavazi na vipodozi visiwani Zanzibar," amesema Dullyzo
Amewaasa
vijana wa visiwani humo kuchakarika na kujihusisha na kazi yoyote ile
ya hali ili kujikwamua kiuchumi na kujiepusha na vitendo viovu
vinavyoiathiri jamii kiujumla kama ubakaji,uporaji na uhalifu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...