Na Editha Karlo wa blog ya jamii Kigoma.

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga amewataka wakazi wa Kigoma kuacha tabia ya kuharibu miundombinu ya barabara ili Makao makuu ya Mkoa yasiwe kama kijiji.

Maganga ameyasema hayo leo round about ya Mwanga kwenye zoezi la uzinduzi wa picha ya sanamu ya samaki aina ya mgebuka kama utambulisho wa rasilimali kwa wageni kwa Mkoa wa Kigoma.

Alisema baadhi ya wakazi Kigoma siyo waaminifu wamekuwa wakifanya uhalifu wa kuharibu miundombinu ya barabara iliyowekwa na serekali kwa gharama kubwa hali inayofanya mji kushindwa kuendelea na kuwa wa kisasa.

"Serikali yetu imekuwa ikitumia fedha nyingi kuboresha miundombinu ya barabara lakini kuna wahalifu wachache wamekuwa wakiharibu miundombinu hiyo,tulifunga za sora za barabarani zikaibiwa mji ukawa giza,yeyote atakayekamatwa anaharibu miundombinu hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake."alisema Maganga

Maganga pia amewataka wakazi wa Kigoma kutunza mazingira kwa kuweka maeneo yao ya makazi na biashara kuwa safi,pia kuacha tabia ya kuacha mifugo inazagaa ovyo mitaani na barabarani.

"Mji wetu umekuwa kama kijiji ukipita mitaani mitaro ya maji machafu,mifugo inazagaa ovyo mitaani,tuutunze mji wetu uwe wa kisasa pia naagiza wafanyabiashara wote waache kufunga maduka saa 12,biashara zifanyike hadi saa sita ikiwezekana hadi asubuhi nina wahakikishia kuwepo kwa ulinzi wa kutosha"alisema

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Hanga amewataka pia wakazi wa Kigoma kutunza picha ya rasilimali ya samaki aina ya mgebuka iliyozinduliwa leo kama alama ya utambulisho wa Mkoa wa Kigoma.

"Sanamu huyu amegharamiwa pesa nyingi kutengenezwa nawaomba sana tuitunze ili iweze kudumu,wakati ujenzi unaendelea hapa tuliifunika na turubai lakini kuna watu waliiba lile turubai tukiwakamata hatutawaoenea haya"alisema Mkuu wa Wilaya.

Meneja wa Tanroad wa Mkoa wa Kigoma Injinia Nalis Choma alisema mradi wa kujenga sanamu ya picha ya mgebuka umegharimu jumla ya shilingi za kitanzania milioni 7 huku milioni 187 zikigharimu ujenzi wa barabara mzunguko(round about)pamoja na mataa.

Choma alisema kuwa wanatekeleza maagizo ya serikali ya kuboresha barabara za Tanroad.

 Wakazi wa Kigoma wakiangalia Picha ya sanamu ya samaki aina ya Mgebuka iliyozinduliwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga kwenye mzunguko wa barabara(round about)ya Mwanga ikiwa kama ishara ya moja ya rasilimali zinazopatikana Mkoani humo
Wakazi wa Kigoma wakipiga picha ya sanamu ya picha ya samaki aina ya mgebuka baada ya kuzinduliwa leo


 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma akikata utepe kuashiria uzinduzi wa sanamu ya picha ya Mgebuka kwenye round about ya Mwanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...