Naibu waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia William Olenasha akizungumza na waandishi wa habari leo alipohudhuria mkutano wa waratibu Kimataifa NGO'Swa nchi mbalimbali zinazotekeleza miradi kwa ushirikiano wa IAEC. Picha zote na Vero Ignatus

Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki nchi profesa Lazaro Busagala akizungumza  na waandishi wa habari katika mkutano wa waratibu wa nchi mbalimbali zinazotekeleza miradi kwa ishirikiano wa IAEC

Mkurugenzi  wa Afrika katika Shirika la International Atomic Agency Profesa Shaukat Abdulrazak akizungumza na waandishi wa habari
Naibu Waziri Elimu Sayansi na Teknolojia Willium Olenasha akizungumza katika mkutano wa waratibu wa nchi mbalimbali zinazotekeleza miradi kwa ishirikiano wa IAEC

Washiriki wa mkutano wa waratibu wa nchi mbalimbali zinazotekeleza miradi kwa ishirikiano wa kama wanavyoonekana pichani
Washiriki wa mkutano huo kutoka Nigeria, Namibia, Morocco
Washiriki kutoka Libya, Kenya 
Washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Central African Republic, Congo
Picha ya pamoja ya mkutano wa waratibu wa nchi mbalimbali zinazotekeleza miradi kwa ishirikiano wa IAEC


Na. Vero Ignatus, Arusha.



Mkutano wa wanachama wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za atomu International Atomic Energy Agency IAEA kanda ya Afrika  umeanza rasmi Mkoani Arusha.



Taarifa inasema kuwa lengo la Mkutano huo ni kujadili namna ya kuboresha ushirikiano katika kusimamia utekelezaji wa Miradi ya Matumizi salama ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia katika nchi wanachama.



Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolijia William Ole Nasha amesema Tanzania imekuwa ikishiriki katika Miradi ya kudhibiti na kuhamasisha Matumizi Salama ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia zinazofadhiliwa na Shirika hilo la IAEA.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Atomu Tanzania Profesa Lazaro Busagala amesema Tanzania imendelea  kunufaika na Miradi mbalimbali ambayo imesaidia  kuboresha  sekta ya Kilimo,Afya, Mifugo, Maji, Rasilimali watu  nishati na Viwanda kutoka Shirika hilo.

Aidha amesema kuwa Miradi hiyo inayo tekelezwa sasa iko Saba na inathamani ya zidi ya bilioni 9.


Mkurugenzi huyo amesema kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 Shirika la IAEA liliisaidia Tanzania kwa kuipatia vifaa vya uchunguzi na Tiba ya Maradhi ya Saratani.



Amesema vifaa hivyo  vimefungwa  katika hospital ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando, na Hospital ya Ocen Road pamoja na vifaa vya Maabara vilivyo gharimu billion 6.2.



Hata hivyi Mkutano umehudhuliwa  na washiriki 46 Kutoka nchi 46 ambao ni wanachama wa Shirika la kimataifa la Nguvu za Atom na unatarijia kuisha tarehe 15 mwezi huu wa Tatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...