Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 15 ambavyo vitatumika katika vyumba vya upasuaji kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye vidonda.
Vifaa hivyo Caiman Lerrafuse HF Generator (GN 200) pamoja na Infovac Therapy System vimetolewa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya kina mama Prof. Sang Lyun Nam akiwa na Daktari Bingwa wa upasuaji ubongo na mishipa ya fahamu Prof. Seung -Kon Huh kutoka Korea Kusini.
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru amesema vifaa hivyo vitasaidia utendaji kazi katika vyumba vya upasuaji, na kuongeza kuwa watalaam hao mbali na kutoa vifaa hivyo lakini pia wanafanya kazi na watalaam wa Hospitali ya Mloganzila hatua ambayo inasaidia wataalam wa hospitali hiyo kupata ujuzi zaidi.
“Wataalam hawa tupo nao hapa Mloganzila na wapo tayari kufundisha watanzania kufanya upasuaji ambao hatufanyi, hata msaada huu waliotupatia ni jitihada zao wenyewe, hivyo napenda kutumia fursa hii kuwashukuru sana kwa msaada huu wa vifaa tiba ambavyo tutatumia ipasavyo kama ilivyokusudiwa”. Amesema Prof. Museru.
Aidha Mkurugenzi huyo Mtendaji wa MNH amesema wanakamilisha mipango ya kuomba watalaam kutoka Korea ili waje kufanya kazi kwa muda na wataalam wa Muhimbili kwa lengo la kuwajengea uwezo katika maeneo mbalimbali ili kuendelea kutoa huduma bora na za kibingwa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru, (wa pili kutoka kushoto) akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Prof Sang Lyun Nam, (kulia) ni Prof. Seung –Kon Huh wa Korea Kusini. kushoto ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzila Dkt. Julieth Magandi akishuhudia makabidhiano hayo.

 Vifaa tiba Caiman Lerrafuse HF Generator (GN 200) pamoja na Infovac therapy system ambavyo vimetolewa kwa ajili ya Hospitali ya Mloganzila.


Prof Lawrence Museru (wa pili kutoka kushoto) akitoa neno la shukrani baada ya kupokea vifaa tiba ambavyo vitatumika katika vyumba vya upasuaji kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye vidonda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...