Msaada wa Chakula, Dawa, magodoro, shuka, blanketi na vyandarua vimewasili Mjini Beira nchini Msumbiji ambako vitagawiwa kwa waathirika wa kimbunga Idai kilichosababisha mafuriko na vifo vya watu zaidi ya 2,000 katika mji huo. Msaada huo ambao umetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli umepelekwa na ndege za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ((JWTZ).
Ndege ya JWTZ ikiwa na misaada wa Chakula, Dawa, magodoro, shuka, blanketi na vyandarua ikiwasili Mjini Beira nchini Msumbiji 
Msaada wa Chakula, Dawa, magodoro, shuka, blanketi na vyandarua vimewasili Mjini Beira nchini Msumbiji ambako vitagawiwa kwa waathirika wa kimbunga Idai k 
Msaada wa Chakula, Dawa, magodoro, shuka, blanketi na vyandarua vikishushwa  Mjini Beira nchini Msumbiji ambako vitagawiwa kwa waathirika wa kimbunga Idai  
Msaada wa Chakula, Dawa na vifaa vya kujihifadhi umewasili Harare nchini Zimbabwe baada ya kupelekwa na ndege za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ} kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa maafa yaliyosababishwa na kimbunga Idai  ambacho kimeikumba sehemu ya nchi hiyo.
Pamoja na kusababisha mafuriko, vifo na maelfu ya kaya kukosa makazi, kimbunga hicho kimesababisha kaya nyingi kuhitaji chakula, dawa na mahali pa kujihifadhi kwa haraka.
Nchi nyingine zilizokumbwa na kimbunga hicho ni Msumbiji na Malawi ambako maelfu ya watu wamepoteza maisha na mamilioni kukosa makazi.

Jana Machi 19, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alitoa msaada wa tani 214 za chakula, Dawa tani 24 na vifaa vya kujihifadhi vikiwemo blanketi, shuka, vyandarua na magodoro ambavyo vilipelekwa katika nchi hizo kwa ndege na Malori ya Jeshi.
Msaada wa Chakula, Dawa na vifaa vya kujihifadhi vikishushwa mjini Harare nchini Zimbabwe baada ya kupelekwa na ndege za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ} kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa maafa


Makabidhiano ya saada wa Chakula, Dawa na vifaa vya kujihifadhi mjini Harare nchini Zimbabwe baada ya kupelekwa na ndege za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ} kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa maafa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...