NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 
MKUU wa wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, Assumpter Mshama amewaagiza watendaji wa vijiji na kata, kuhakikisha watoto wa wafugaji walio na umri wa kwenda shule, wanakwenda ili wapate haki ya elimu kama ilivyo kwa watoto wa jamii nyingine. 

Aidha ameeleza, wilaya inatarajia kuchukua sensa ya watoto wa wafugaji ili kupata idadi kamili ya watoto hao ambao hawaendi shule hadi sasa. 

Assumpter alitoa agizo hilo, wakati akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha wafugaji na wakulima, kijiji cha Kwala, Kibaha Vijijini. 

Aliwataka ,wafugaji kuacha kuwatumikisha watoto wao kuchunga mifugo hasa ng'ombe badala ya kuwapeleka shule kupata elimu. 

"Watendaji nendeni mkahakikishe hakuna mtoto wa mfugaji anaefuga, hawa ndio Sokoine wa kesho, kwenye maziwa kuna akili, wanarubuniwa tuu, ila wafugaji watie akilini kwamba mtoto akizaliwa sio wako ni mali ya serikali "

"Haiwezekani wewe unaenjoy, mnakaa kujiolea wanawake 30, wakati watoto wako hawaendi shule, baadae hawa hawajui kama wataweza kuoa wake wengi hivyo kutokana na uchumi na maisha yanavyobadilika ""alisema Assumpter. 

Mkuu huyo wa wilaya alielezea, serikali inajitahidi kujenga mazingira bora ya kielimu na kusomesha watoto bure kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha nne lakini jamii hiyo haijatambua umuhimu wa fursa hiyo. 

Pamoja na hayo,Assumpter aliwaomba waendelee kuheshimiana ,kuishi kwa upendo kati ya jamii ya wafugaji na wakulima .

Nae makamu mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT) Esta Moreto aliiasa jamii hiyo kujenga utamaduni wa kusomesha watoto wao badala ya kuwageuza wachungaji wa mifugo ya familia, bali wafanye shughuli hiyo baada ya kutoka masomoni. 
MKUU wa wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, Assumpter Mshama 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...