Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe (katikati) akisoma maelezo leo kwenye sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mjini Tabora wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Tabora ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza na wananchi leo kwenye sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mjini Tabora wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Tabora ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na watumishi na viongozi mbalimbali leo wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Tabora ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.



Baadhi ya watumishi na viongozi wa Manispaa ya Tabora wakimsikiliza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha ) wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Tabora ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.



Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe (kulia) akisalimiana na watumishi leo wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Tabora ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.
Picha na Tiganya Vincent

……………..

NA TIGANYA VINCENT

SERIKALI imewataka wananchi kuacha tabia ya kuharibu maeneo ya kihistoria ikiwemo majengo ya kale kwa madai potofu kuwa kwenye maeneo hayo wakoloni walificha madini ndani yake.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Tabora ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.

Alisema vitendo vya aina hiyo vinasababisha Serikali kutumia gharama kubwa pindi wanapotaka kukarabati na kurudisha historia ya maeneo hayo.

“Hakuna ambaye ni mjinga aweke ndani ya nyumba dhahabu halafu asiifuate…hata wangekuwa wameweka mali ndani ya majengo yao wamekuja na njia nyingine ya kutaka kuendeleza maeneo hayo kwa kuweka miradi ya kuchimba visima ili wachukue madini kama yangekuwepo” alisema.

Mwakyembe alisema maeneo hayo ni muhimu sana katika Historia ya Tanzania na pia katika ukuzaji wa utalii kwa ajili ya kulipatia Taifa fedha za kigeni. Aliongeza kuwa maeneo hayo ni muhimu katika kutoa elimu kwa vijana wa kitaifa kufahamu historia ya nchi yao kwa ajili ya kuwa wazalendo wazuri wa Tanzania. Mwakyembe alisema Wizara yake inaewndelea na utaratibu wa kuyaorodhesha maeneo yote ya kihistoria kwa ajili ya kuyahifadhi na kuyakarabati kwa ajili faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

Aidha Waziri huyo alisema Serikali iko mbioni kupeleka Bungeni Muswada wa Sheria ambayo utafanya maeneo ya kihistoria yasiguswe na kuzuia uharibifu. Alisema baada ya muswada huo kupitishwa na hatimaye kuwa Sheria utasaidia kulinda utajiri wa urithi wa Kihistoria ulipo hapa nchini usiweze kuharibiwa na kupotea. Katika hatua nyingine Mwakyembe alisema Serikali itahakikisha inarudisha nchini Fuvu la Kichwa cha Mama Shujaa mpiga ukoloni wa Kijerumani kutoka Singida Bibi Liti.

Alisema Shujaa huyo aliweze kupambana na Wajerumani kwa kutumia nyuki hadi hapo aliposalitiwa na wenzake na hatimaye Wajerumani wakata kichwa chake na kuondoka nacho.

Mwakyembe alisema lazima fuvu la kichwa lirudishwe nchini na kuhifadhiwa katika jumba maalumu kwa ajili ya historia ya Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...