*Ni baada ya kufurahishwa na mafunzo yanayotolewa na Puma Energy Tanzania kwa wanafunzi wa shule za msingi

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Energy, imezindua mafunzo na uchoraji la usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi, mafunzo ambayo yatawapa uelewa wa usalama huku Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamadi Masauni akitoa ombi kwa Puma kutoa elimu hiyo kwa shule zote nchini.

Uzinduzi huo umefanyika leo Machi 18 , 2019 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Yussuf Masauni, ambapo Mkurugenzi wa Puma, Dominic Dhanah, amefafanua mafunzo hayo yanakwenda sambamba pia kwa wanafunzi waliowahi kufundishwa.

Amesema madhumuni ya kuwahusisha wanafunzi wa shule za msingi ni kutokana na imani yao kwamba, watoto hao wanakabiliwa na hatari za ajali za barabarani na kuhitaji mafunzo ya usalama barabarani ili kuepukana na ajali.

“Usalama barabarani ni kipaumbele namba moja katika Kampuni ya Mafuta Puma na tumeamua kuwafundisha watoto wadogo kwani tunfahamu hatari za barabarani wanazokabiliana nazo. Kampuni ya Puma inafanya biashara ya mafuta katika nchi 49 duniani na kwa Afrika tupo katika nchi 19. Mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi yalianza mwaka 2013 hapa Tanzania na mpaka sasa shule 75 zimenufaika na mafunzo haya wakati wanafunzi 80,000 wamepata mafunzo haya,"amesema

Ameongeza kuwa "Tumefanya utafiti na kugundua kuwa shule tulizoendesha mafunzo haya , ajali kwa wanafunzi zimepungua na hivyo basi kwa mwaka 2019 mafunzo haya yataendeshwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar,” alisema Dhanah

Kwa upande wake Naibu Waziri Masauni, amesema Serikali inafarijika na kazi inayofanywa na Kampuni ya Puma kwa kurudisha faida inayopatikana kwa jamii ikiwamo kutoa mafunzo muhimu ya usalama barabarani.

Amesema elimu ni suala la kipaumbele kwa jamii na mkakati wa wao Wizara ya Mambo ya Ndani na Serikali kwa ujumla ni kupunguza ajali za barabarani na Puma inafanyakazi hii kwa karibu na Machi 30, mwaka huu tutakuwa na kongamano la wiki ya usalama barabarani pia tujadili hili kwa kina.

"Serikali tunatambua kazi nzuri ambayo inafanywa na Puma Energy Tanzania katika kutoa elimu hii inayohusu usalama barabarani.Ni jukumu letu na wananchi kwa ujumla kuunga mkono jitihada hizi.,” alisema Masauni

Akifafanua zaidi Mhandisi Masauni amesema kitendo cha Puma kuwa na programu hiyo kinaonesha namna ambavyo wanakataa ajali za barabarani kwa vitendo na kwamba wanafunzi ambao wanapata elimu hiyo anauhakika watakuwa mabalozi wazuri wa kuelezea kwa usahihi mtembea kwa miguu anatakiwa kufanya nini akiwa barabarani.

"Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha Usalama Barabarani wana program nyingi za kusaidia kutoa mafunzo kwa shule zote zilipo kwenye mazingira hatarishi na zisizo kwenye mazingira hayo pia. Programu hizo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto mbalimbali za kifedha. Ninaomba kutumia fursa hii kuomba uongozi wa Puma kukisaidia Kikosi cha Usalama Barabarani kuzifikia shule zote nchini kwa kupitia askati walioko kwenye maeneo yote nchini,"amesema Pia amemuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani kuanza mchakato wa kuandaa andiko la kutoa mafunzo kwa shule zote nchini na kuliwasilisha kwenu (Puma) ili muone namna yambavyo mnaweza kusaidia kuokoa kizazi chetu cha kesho,” amesema Masauni.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akimpa zawadi mmoja wa Wanafunzi wa shule ya msingi Bunge jijini Dar,mara baada kujibu vizuri swali lililohusu mambo ya usalama barabarani,kabla ya ufunguzi rasmi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania iishirikiana na wadau wengine ikiwemo taasisi ya AMEND.
Mmoja wa Watoa Mafunzo ya Usalama barabarani kwa Wanafunzi wa shule ya msingi chini ya Ufadhili wa kampuni ya Puma Energy Tanzania,Neema Swai kutoka taasisi ya AMEND akionesha moja ya mchoro ulioshinda kwenye shindano la Wachoraji kuhusu Usalama barabarani mwaka 2018,mbele ya mbele ya Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi ( wa pili kulia ) Mhandisi Hamad Masauni,wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na kampuni ya Puma Energy Tanzania
Ufunguzi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ukiendelea leo jijini Dar

Mwanafunzi Shule ya Msingi Bunge jijini Dar, Omari akifafanua kuhusu namna ya matumizi sahihi kwa watembea kwa miguu mbele ya Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchi ( wa tatu kulia ) Mhandisi Hamad Masauni,wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na kampuni ya Puma Energy Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania,Dominic Dhannah akizungumza leo jijini Dar wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na kampuni hiyo,ambapo mgeni rasmi ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi ( wa kwanza kulia ) Mhandisi Hamad Masauni
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na kampuni ya Puma Energy Tanzania kishirikiana na wadau wengine ikiwemo taasisi ya AMEND.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania akiwa na baadhi ya Wanafunzi ambao ni pia ni Mabalozi wa shule ya msingi Bunge jijini Dar,ambao wamehudhuria ufunguzi wa mafunzo ya usalama barabarani yanayotolewa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania kishirikiana na wadau wengine ikiwemo taasisi ya AMEND.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhandisi Hamad Masauni akiwaaaga baadhi ya wanafunzi ambao ni pia ni Mabalozi wa Usalama barabarani wa shule ya msingi Bunge jijini Dar,mara baada ya kufungua rasmi mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na kampuni ya Puma Energy Tanzania kishirikiana na wadau wengine ikiwemo taasisi ya AMEND.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...