*Uwanja wa Taifa kwa Mkapa kumenoga...Simba full tambo

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

UWANJA wa Taifa jijini Dar es Salaam kumenoga!Hakuna maneno mengine ya kuelezea zaidi ya hayo wakati Tanzania ikitarajia kusimama kwa dakika 90 kushuhudia mechi kati ya Simba FC na AS Vita ya nchini Congo.

Wakati mchezo huo ukitarajiwa kuanza saa 1:00 kamili ya usiku ya leo Machi 16,2019 idadi kubwa ya mashabiki na wapenzi wa soka hasa wa Simba wamejitokeza kwa wingi kwani licha ya mchezo huo kuanza muda huo sehemu kubwa ya uwanja  umeanza kujaa.

Shangwe na nderembo zilizoambatana na tambo kwa mashabiki wa Simba zimetawala uwanjani hapa .Mashabiki wa Simba wakijipa matumaini wa kuondoka na alama tatu muhimu za mchezo  huo.

Kwa kukumbusha wakati Simba wakijigamba kushinda mechi ya leo katika mchezo wa awali uliofanyika nchini Congo Simba walipokea kichapo cha mabao 5-0.Hata hivyo mashabiki wa Simba wanasema uzuri wa mechi hizi  kila timu inauhakika wa kushinda nyumbani.Acha tusubiri.Simba shusheni presha.

Pamoja na tambo za Simba ukweli utabaki kwamba dakika 90 zitaamua nani anakwenda hatua ya robo fainali ya ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Baadhi ya mashabiki wa Simba wameiambia Michuzi Blog jioni hii uwanjani hapa kwamba kwa mapenzi ya Mungu watashinda mechi yao dhidi ya AS Vita na kushinda kwao kutaongeza idadi ya timu zitakazoshiriki mwakani na kubwa zaidi in heshima kwa nchi.

Wakati Simba wakijiaminisha hivyo baadhi ya mashabiki wa Yanga walioko uwanjani hapa akiwemo Moses John na Idd Athuman wamesema Simba kushinda mechi ya leo ni sawa na  Ngamia kupenya kwenye tundu za sindano.Mbona mtihani!Kha!

Nje ya uwanjani idadi ya mashabiki walioko kwenye foleni ya kuingia uwanjani ni kubwa .

Kauli mbiu ya Simba katika mchezo wa leo inasema Do or Die wakiwa na maana kufa au kupona wakiamini kwamba ushindi ndilo jambo pekee wanalolitarajia kuona.

Kwa kukumbisha katika mchezo huo Simba inahitaji kushinda ushindi wa magoli yoyote kwani sare kwao haina maana yoyote na iwapo itatokea watakuwa wameaga mashindano hayo yenye heshima kubwa barani Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...