MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga NHIF umejipanga kuhakikisha inatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na Bima ya afya iliyoboreshwa .

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Mfuko huo  Mkoani Tanga, Ally Mwakababu wakati akizungumza na MTANDAO huu kuhusu walivyojipanga kuhakikisha wanaongeza wananchi na kuboresha huduma zao.

Alisema kuwa iwapo wananchi wataweza kupata uwelewa wa kutosha kuhusu umuhimu wa kuwa na kinga ya matibabu kabla ya kuugua wataweza kuwakomboa wananchi wengi.

“Hakuna mtu au kiongozi ambaye atakuwa tayari kuongoza wananchi ambao ni goigoi wa maradhi hivyo Bima ya afya tumejipanga kuhakikisha kwanza tunaongeza idadi ya wanachama lakini kupitia wao  tutaweza kuboresha huduma katika vituo vya afya”alisema Mwakababu.

Hata hivyo Mwakababu alisema kuwa licha ya mkoa wa Tanga kuwa wapili kwa uandikishaji wa bima ya afya ya jamii CHF  lakini bado eneo hilo hawakuweza kufanya vizuri zaidi hivyo kwa mwaka huu wamejikita katika kuongeza uhamasishaji zaidi.

Alisema kuwa wamejipanga kufanya hamasa kuanzia ngazi ya mkoa hadi vijiji kwa kushirikisha viongozi wa kiserikali na kisiasa kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi ndani ya Tanga anaona umuhimu wa kuwa na kadi ya Bima.

Vile vile akiongelea kadi ya Bima ya Toto afya Mwakababu alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2017/18 waliweka lengo la kuandikisha watoto waliochini ya umri wa miaka 18 ,3000 badala yake waliandikisha 913.

Huku kwa walioko katika ngazi ya sekondari na vyuo ambao wanatumia huduma ya Toto afya kadi waliweza kuandikisha 1435 kati ya malengo waliyojiwekea ya kuandikisha wanachama 3000.

“Tatizo kubwa ni mwamko mdogo wa wananchi kuona umuhimu wa kuwa na bima ya afya  wao wanasubiri mpaka ugonjwa uwe mkubwa  na kushindwa gharama za matibabu lakini kumbe kama wangeweza kujiunga mapema wasiweza kupata huduma bora”alisema Meneja huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...