Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema kuwa imeridhishwa na mtambo wa TTMS wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) unavyofanya kazi katika katika kulinda usalama wa Mawasiliano nchini.

Akizungumza wakati Kamati hiyo ilivyotembelea Mamlaka Hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya PAC Naghenjwa Kaboyoka amesema kuwa wamejiridhisha katika mtambo huo kwa umerahisisha TCRA kufanya kazi kwa ufanisi katika kuweza kusaidia serikali kupata mapato.

Amesema walikuwa na shaka kuhusiana na mtambo huo lakini wamejiridhisha kwa na kuondoa mashaka hayo kwa kamati na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) nao wamejiridhisha na mtambo huo.

Kaboyoka amesema TCRA imepiga hatua nzuri katika mawasiliano kwa kuwa na watendaji mahiri wa kuendesha mtambo huo.

"Uzuri wa mtambo TTMS unasimamiwa na wazawa hii inaoyesha kuwa kila kinachofanyika kitakwenda sawa kuliko mtambo huo ungesimamiwa na watu wa nje"amesema Kaboyoka.Aidha amesema kuwa TCRA iendelee kudhibiti mawasiliano ikiwa ni pamoja na kwenda kukuza uchumi wa nchi.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Mhandisi James Kilaba amesema kuwa mtambo huo unaweza kukokotoa takwimu zote miamala ya fedha unavyofanywa na kampuni za simu kutoka na moja kwenda Mtandao mwingine.Amesema kazi nyingine ni kusimamia simu ndani na nje sambasamba na kutambua simu za ulaghai, uhakiki wa mapato na ubora wa mawasiliano.

Amesema kuanza kwa mfumo huo umesaidia kupunguza simu za ulaghai kutoka asilimia 65 hadi kufikia asilimia 10 ikiwa ni pamoja kuongeza pato la Taifa kwa asilimia 9.8.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Mhandisi James Kilaba akizungumza na kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipotembelea Mamlaka hiyo.
 Afisa wa Makumbusho wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Abdulrahman Milasi akitoa maelezo wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu PAC ilipotembelea Mamlaka hiyo katika Makumbusho ya vitu vilivyotumika zamani katika mawasiliano.
 Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA Dkt Jonas Kilimbe akitoa maelezo kuhusiana na utendaji wa TCRA wakati Kamati ya PAC Ilipotembelea Mamlaka hiyo.
 Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA)Jumanne Ikuja akitoa maelezo katika gari la kuangalia masafa wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali PAC ilipotembelea Mamlaka hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC)  Naghenjwa Kaboyoka akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...