*Mradi wa Nyumba Kigamboni, Gezaulole umegharibu kiasi cha Tsh. Bilioni 21.7
*Mradi wa Bunju B umegharimu Tsh. Bilioni 4.1.


Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeshauri kujengwa huduma za kijamii ikiwemo miundombinu katika ujenzi wa miradi ya nyumba iliyopo Gezaulole, Kigamboni na Bunju B jijini Dar es Salaam.

Miradi ya Ujenzi wa Nyumba hizo unatekelezwa na Watumishi Housing Company, ambapo PAC imefanya ziara maeneo hayo kuangalia ubora wa nyumba hizo, Uuzaji na upangishaji pamoja na kuhakikisha pesa hizo za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii hazitapelekea kufirisi Mifuko hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada yakutembelea miradi hiyo, Mwenyekiti wa PAC, ambaye ni Mbunge wa Same Mashariki, Mhe. Nagy Livingstone Kaboyoka amesema nyumba hizo zinaridhisha kutokana kiasi cha Pesa kilichotumika.

Mhe. Kaboyoka amewashauri Watumishi Housing kuhakikisha Miundombinu bora zikiwemo Barabara, Shule, Zahanati pamoja na Masoko zinapatikana maeneo hayo kwa urahisi ili kuleta kichocheo kutokana na umbali wa nyumba zilipo. 

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aesh Hillary ameungana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo kuridhishwa na Bei za nyumba, Soko licha ya Watumishi wangi kuhamia Dodoma, amesema ujenzi wa nyumba hizo umelenga zaidi Watumishi wa hali ya chini ambapo ameomba mradi huo kuenezwa sehemu mbalimbali nchini. 

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company, Dkt. Fredy Msemwa amesema mradi wa huo umekamilika kwa 95%, Kigamboni, Gezaulole ukikamilika utakuwa na nyumba 795, amesema awamu ya kwanza utakuwa na nyumba 329, ambapo 268 ni Ghorofa na 61 nyumba za chini, 50% ya nyumba hizo tayari zimeuzwa.

Amesema mradi wa ujenzi Bunju B umekamilika kwa 98%, una nyumba 64 pamoja na Miundombinu yote kukamilika ambapo nyumba 20 tayari zimeuzwa.

Dtk. Msemwa amesema Mardi huo utafungua fursa ya mauzo kwa Watumishi wa Umma kwa nyumba hizo, Pia itafungua fursa kwa Sekta binafsi wakiwemo Waandishi wa Habari pamoja na Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Mwenyekiti wa PAC, ambaye ni Mbunge wa Same Mashariki, Mhe. Nagy Livingstone Kaboyoka (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea miradi ya nyumba zilizopo Gezaulole, Kigamboni na Bunju B jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa (wa kwanza kulia) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa PAC, Mhe. Nagy Livingstone Kaboyoka (wa pili kulia) wakati wa ziara ya Kamati hiyo ilipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba wa Gezaulole, Kigamboni jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Mssaka,MMG)
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali wakitembelea Miradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Gezaulole wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa majengo ya Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Gezaulole wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam. 
Muonekano wa majengo ya Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Bunju B wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...