NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania(UWT), Ndugu Gaudensia Kabaka amewataka Akina Mama katika Wilaya ya Dimani kicha Unguja kufanya maandalizi ya kina ya kisiasa yatakayoleta ushindi wa CCM mwaka 2020.

Rai hiyo aliitoa katika ziara yake wakati akiwahutubia Akina Mama wa UWT wa Wilaya hiyo katika Afisi za Umoja huo huko Kiembe Samaki Zanzibar.

Alisema Akina Mama wanatakiwa kujipanga vyema kwa kuhakikisha CCM inashinda na kuendelea kuongoza Dola katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Alieleza kwamba tayari Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa asilimia 97 hivyo kazi iliyobaki, kwa akina Mama hao ni kunadi, kutangaza na kueneza Sera za maendelezo zinazotekeleza na Chama pamoja na Serikali.

Alieleza kuwa maendeleo yaliyopatikana kwa CCM yamechangiwa na busara na nguvu za Akina Mama kwani wameanza harakati za kupigania uhuru na maendeleo ya Nchi toka enzi za ASP na TANU toka Uongozi wa Marehemu Mzee Abeid Karume na Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Aliwambia kuwa ni lazima wanawake waliende hadhi na heshima zao katika kusimamia ukweli na Falsafa za za Uongozi bora zilizoasisiwa na Akina Mama waasisi wa UWT toka ilivyoanzishwa.

Alisema kuwa pamoja na majukumu waliyokuwa nayo katika Medali za Kisiasa ni lazima waendeleze ubunifu katika kufanikisha kwa vitendo Sera ya Siasa na Uchumi Nchini, kwa kufanya ujasiriamali ili wajiongezee kipato.

Akizungumza na Akina Mama wa Kanisa la Anglicana huko Mbweni aliwapongeza kwa juhudi zao za kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi.

Aliwambia kuwa Chama cha CCM hakina ubaguzi wa kidini kwani kinapokea na kufanya kazi na wanachama wa dini zote, hatua inayokitofautisha na Vyama vingine vinavyoanzishwa kwa misingi ya kidini.

Aliwasihi Akina Mama hao kuendeleza umoja na mshikamano wa kudumu kwa kushirikiana katika masuala mbali mbali ya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndungu Thuwaiba Kisasi ameeleza kwamba Akina Mama hao wa kanisa la Anglicana wamekuwa wanachama waaminifu na wachapakazi kwa kipindi chote na wenye msimamo usioyumba.

Naye Katibu Mkuu wa UWT Taifa Mwl. Queen Mlozi aliwataka wazazi na walezi kusimamia malezi ya Watoto wa Kike ili wapate haki ya Elimu bila vikwazo.

Amesema watoto wa Kike wasiposaidiwa na kulelewa katika mazingira salama hapatopatikana wataalamu na viongozi jasiri na wachapakazi nchini hivyo wanastahiki kulindwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi Ndugu Zainab Ali Maulid, alisema wanawake wa Mkoa huo wamekuwa mabalozi waaminifu wa kulinda na kutetea maslahi ya CCM kwa vitendo.

Katika risala ya Wilaya hiyo Akina Mama hao wamesema CCM imeendelea kuwa na mvuto na kupendwa na wananchi kutokana na Utekelezaji Mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 inayotekelezwa vyema kwa wananchi wote.
 MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akikagua bidhaa zinazotengenezwa na Akina Mama wa Kanisa la Anglicana huko Mbweni Zanzibar.
 WANAWAKE wa Kanisa la Anglicana wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia Kabaka aliyefika katika Kanisa hilo kwa ajili ya kuwasalimia Akina Mama hao na kukagua vikundi vya ujasiriamali.
 MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akivishwa sikafu na Vijana wa Kikundi Maalum cha UVCCM Wilaya ya Dimani Kichama Unguja mara baada ya kuwasili katika Afisi za Wilaya hiyo kwa ajili ya ziara.
WANAWAKE wa UWT wakiwa Katika ukumbi wa  Afisi ya UWT  Kiembesamaki wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti  wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka katika Kikao cha ndani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...