Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, mchoro wa jengo la Ofisi za Wizara ya Mambo ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zinazojengwa kwenye Mji wa Serikali uliopo Mtumba, Dodoma. Makabidhiano hayo yalifanyika tarehe 12 Machi 2019. Baada ya kukabidhiwa Prof. Kabudi alipongeza jitihada za Wizara chini ya usimamizi wa Mhe. Dkt. Mahiga kwa hatua kubwa iliyofikiwa kwenye ujenzi huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome akitoa maelezo mafupi kwa Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria walipofika  kwenye ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria zinazojengwa kwenye mji wa Serikali uliopo, Mtumba jijini Dodoma kwa ajili ya makabidhiano.
Mhe. Prof. Kabudi na Mhe. Dkt. Mahiga wakiwa kwenye moja ya chumba cha jengo la  ofisi za Wizara  zinazojengwa Mtumba


Mhe. Prof. Kabudi akisalimiana na mmoja wa Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alipotembelea ofisi za Wizara zinazojengwa Mtumba
Mhe. Prof. Kabudi akiongozana na Mhe. Dkt. Mahiga kuelekea kwenye jengo la Wizara, Mtumba
Mhe. Prof. Kabudi akisaini kitabu cha wageni na kutoa maoni yake kuhusu maendeleao ya ujenzi  wa ofisi hizo 
Mhe. Prof. Kabudi na Mhe. Dkt. Mahiga wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo na mafundi wanaojenga jengo la ofisi za Wizara zilizopo Mtumba
Muonekano wa jengo la ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki linalojengwa kwenye mji wa Serikali uliopo Mtumba, DodomaWaziri wa Katiba na Sheria ambaye awali alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akikabidhi Taarifa ya Makabidhiano ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.  Prof. Palamagamba Kabudi ambaye awali alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dodoma tarehe 12 Machi 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto) akimkabidhi Taarifa ya Makabidhiano ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiweka saini Kitabu cha mahudhurio mara baada ya kukabidhiwa ofisi jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi mara baada ya makabidhiano ya ofisi.
Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakishuhudia makabidhiano ya ofisi kati ya Waziri wa Katiba na Sheria na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiongea na Wakuu wa Idara na Vitengo (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa ofisi na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga.
Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hayupo pichani).
Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiongea na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi Savera Kazaura akitoa maelezo kwa  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Waziri wa Katiba na Sheria kabla zoezi la makabidhiano kuanza.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akisalimiana na baadhi ya watumishi mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Anayemkaribisha  ni mmoja wa watumishi hao, Bw. Shaban Mtambo.
Bi. Chiku Kiguhe akisalimiana na Mhe. Prof. Kabudi.
Bw. Habibu Ibrahim akisalimiana na Mhe. Waziri.
Bw. Maulidi Mkenda akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiongea na baadhi ya watumishi waliojitokeza kumpokea mara alipowasili kwa mara ya kwanza katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje jijini Dodoma.
Bw. Caesar Waitara akisalimiana na Mhe. Prof. Kabudi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...