Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habari katika mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kuwatembelea wananchi ili kuwasikiliza na kujua ukweli kuhusiana na sakata la maji mkoani hapo. Picha na Vero Ignatus.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira,Mhandisi Ruthy Koya akiongea na waandishi wa habari ambapo amesema wataalam wamechunguza maji hayo na kubaini kuwa hayana tatizo na kusisisitiza wananchi kuendelea kuyatumia kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Ghambo, kushoto kwake ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Hospitali ya Mkoa ,Dk,Omary Chande
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimsikiliza mmoja wa wazee katika baadhi ya mitaa aliyoitembelea.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrosho Gambo akinywa maji kwenye moja ya kaya aliyoitembelea ambapo maji hayo wananchi wamekuwa akiyashuku kuwa siyo salama,na kuwahakikishia kuwa ni salama na hayana tatizo.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira,(AUWSA) Mhandisi Ruth Koya akinywa maji ambayo wananchi wameyatilia shaka kwamba siyo safi na salamaamewahakikishia kuwa maji hayo hayana tatizo na kusisisitiza wananchi kuendelea kuyatumia, huku akisisitiza wayachemshe na kuyachuja vizuri
Mtaalamu wa vipimo katika kutoka wizara ya maji mahabara ya kituo Arusha ambapo ndipo maji yapimwa. na kujiridhisha kuwa maji ni safi na salama na yana dawa ya kutosha, mkuu wa Mkoa akipewa maelekezo namna inavyofanya kazi


Na. Vero Ignatus, Arusha.


Ile sintofahamu ya wakazi wa Jiji la Arusha kuendelea kupata homa ya matumbo kutokana kudaiwa kunywa maji yaliyochanganyikana na maji taka limechukua sura Mpya Mara baada ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kutembelea kaya zilizoathirika huku akinywa maji hayo kwa lengo la kujiridhisha na kubaini maji hayo hayana madhara

Akiongea na wananchi katika Kata ya Themi Gambo alikiri kuwa baadhi ya wananchi wamekumbwa na tatizo la kuumwa matumbo na kuhara ndiyo maana wao kama serikali wameamua kuwatembelea na ili kujiridhisha kuwasikiliza

Katika ziara hiyo Mhe. Gambo aliambatana na wataalamu wa Afya Mkoa wa Arusha Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira ,kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa

Mitaa ambayo wameitembelea ni pamoja na mitaa ya Naura Kata ya kati ,Mtaa wa Ndarvoi kata ya Daraja mbili na Kata ya Themi ambapo wananchi walimweleza ambapo wananchi waliweza kumueleza wa mkoa jinsi walivyoathirika na kunywa maji hayo waliodai yamekuwa na harufu kali ya kinyesi.

Wananchi hao ,Boniface Chacha,Jesta John na Hawa Hasan wamesema maji ya bomba wanayokunywa ni changamoto kubwa kwao na kuitaka serikali iwasaidie kuhakikisha afya zao hazidhuriki kutokana na matumizi ya maji safi wanayotumia."Nimetembelea eneo moja baada ya nyingine kujionea tatizo la maji na nikiri kweli kunabaadhi ya watu wanaumwa matumbo na bado wataalam wanachunguza suala hili lakini nasisitiza hakuna uchafuzi wa maji safi kuingiliana na maji taka"

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Hospitali ya Mkoa ,Dk,Omary Chande amesema madaktari wamechukua sampuli za maji na wanaendelea kuzipima kwenye maabara na hakuna mgonjwa yoyote aliyelazwa hospitali ya mkoa bali Jiji kwa maana ya vituo vya afya wamepokea wagonjwa 310

Dkt. Chande amesema sampuli mbalimbali zinaendelea kuchunguzwa ili kubaini ni kitu gani kimesababisha watu kuumwa matumbo

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira,Mhandisi Ruthy Koya amesema wataalam wamechunguza maji hayo na kubaini kuwa hayana tatizo na kusisisitiza wananchi kuendelea kuyatumia na wale wasiyotumia maji hayo wachemshe maji


Amesema baada ya kuoana taarifa Mamlaka waliweza kutembelea sehemu husika zinazolalamikiwa na kuchukua sampuli na kuwashirikisha wenzao wizara ya maji mahabara Arusha na kujiridhisha kuwa maji ni safi na salama na yana dawa ya kutosha

Amesema AUWSA hawajaweza kukidhi uhitaji wa maji katika jiji la Arusha kwa 100%kwani,upatikanaji wa maji ni 40%kwahiyo ile 60%inakuwa inajazilushiwa na watu binafsi kwa vyanzo vyao tofauti

Natoa shukrani nyingi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na serikali yake shukrani kwani ametoa fedha nyingi kwaajili ya kuondoa tatizo la maji Jijini Arusha

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Shana ametoa onyo kwa mtu yeyote yule ambae atasambaza habari za uchochezi au mtu yotote atakayeeneza uvumi wa maji safi kuchanganyika na maji taka atachukuliwa hatua za kisheria kwani tayari ufafanuzi wa kina umeshatolewa na mamlaka husika 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...