Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga amewataka vijana mkoani Kigoma kuacha wizi wa miundombinu ya Serikali na kwa atakayekamatwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Hayo aliyasema leo wakati wa uzinduzi wa Sanamu ya Samaki aina ya Mgebuka ambapo alisema kumekuwa na tabia ya vijana wengi kuiba taa za barabarani na wengine kuvamia majimbani na kuiba, na kuwataka waache tabia hiyo na kufanya kazi.

Aidha Mkuu huyo alisema kuanzia sasa wafanyabiashara mkoani Kigoma waanze kufanya hadi saa sita usiku tofauti na mwanzo ambapo walikuwa wakifunga maduka yao saa kumi na mbili jioni kwa kuwa ulinzi umeboreshwa mkoani Kigoma na Miundombinu imeboresha kwa kuwa Serikali imejipanga kuwasaidia Wananchi kuleta maendeleo.

Alisema Kwa yeyeto atakayekamatwa akijihusisha na ujambazi hawatamvumilia, na kutoa onyo kwa kikundi cha vijana kinacho jishughulisha na masuala ya ubakaji na wizi kuacha maramoja na endapo watakamatwa serikali itawachukulia hatua .

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa barabara was Barabara nchini Tanzania( TANROADS) Naris Choma alisema,ujenzi wa sanamu ya Samaki ni maagizo ya Serikali kwamba barabara zote zinazo hudumiwa na TANROADS kuboreshwa iliziweze kuwa na maadhari nzuri na ziweze kuwahudumia wananchi.

"Na leo wameanza na sanamu ya Mgebuka inaashiria ni samaki anaepatikana katika Ziwa Tanganyika na kwa heshima ya Wakazi wa Kigoma kuweka Sanamu hii kuonyesha vivutio vilivyopo mkoani Kigoma,", amesema.

Alisema ujenzi wa sanamu umegharimu kiasi cha shilingi milioni saba na laki moja na umeambatana na mzunguko ambao nao umeghalimu kiasi cha shilingi milioni 187 pamoja na taa.

Pia wanatarajia kufanya Upanuzi wa mifereji na upanuzi wa barabara, ujenzi wa daraja la waenda kwa miguu katika Soko la Kigoma kupunguza msongamano wa Watu na Magari.

Nao baadhi ya Wananchi akiwemo Alex Dackriss alisema hatua hiyo ni nzuri na wameipongeza Serikali kwa kujenga sanamu hiyo kwa kuwa walizoe kuona smaki Mwanza na wanaahidi kuitunza miundombinu hiyo kwa kuwafichua wote watakao baini wanafanya wizi wa miundombinu ya Serikali.

Juma Kizza nae ni mkazi wa Kigoma alisema Wamefarijika kuona mgebuka na maendeleo ya naendelea mkoani Kigoma na kuwaomba Vijana wafanye kazi na kuacha kuiba miundombinu ambayo inawasaidia wenyewe.

Alisema Suala la kufanya biashara hadi usiku wanampongeza Mkuu wa Mkoa wa uamuzi huo na kuomba ulinzi kuimalishwa na kuboresha miundombinu itakayo ruhusu biashara kufanyika.
 Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo 
 
 Wanachi wakishngilia baada ya kufanyika uzinduzi huo
  Sanamu yasamaki aina  mgebuka baada ya kuzinduliwa rasmi
MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga kwa pamoja wakikata utepe kuzindua  Sanamu ya Samaki aina ya Mgebuka ambapo alisema kumekuwa na tabia ya vijana wengi kuiba taa za barabarani na wengine kuvamia majumbani na kuiba, na kuwataka waache tabia hiyo na badala yake wajitume kufanya kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...