Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda katika kuwawezesha watoto wa kike waliokuwa wanafaulu vizuri masomo ya sayansi lakini wanashindwa kuendelea na masomo, kwasababu ya ugumu wa maisha ameamua kuunda mfuko maalumu utakaokuwa na jukumu la kusomesha wasichana 100 Bure kila mwaka kuanzia kidato cha tano hadi sita.

RC Makonda amesema walengwa wa Mfuko huo ni watoto wa kike waliofaulu vizuri masomo ya sayansi licha ya kutokea kwenye familia duni ambazo ni yatima, watoto wa Mamantilie, kondakta,wavuvi na ombaomba.

Aidha RC Makonda lengo la kujikita kwenye masomo ya sayansi ni kuzalisha Madakrari bingwa wanawake, Marubani, wabobezi wa computer, wataalamu wa gesi na fani nyinginezo ambazo anaamini ukimkomboa mwanamke umeikomboa jamii.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema waliopata fursa hiyo watagharamiwa kuanzia Ada, Madaftari, Bag,Vitabu na pesa ya kujikimu ili wabaki ni jukumu moja la kusoma na kufaulu. 

Mhe. Makonda amesema hatua hiyo inaenda sambamba na kuunga mkono jitiada za Rais Magufuli kupambana na umaskini kwa kuhakikisha watoto wa maskini wanasoma bure ili waje kuzisaidia familia zao.

RC Makonda anaamini kuwa kama mtoto wa kike ameweza kufaulu masomo na kuvishinda vishawishi vya mafataki wanaotumia pesa au lifti kuwarubuni na kuwapa ujauzito, basi mtoto huyo akiendelezwa anaweza kuwa mtu mkubwa nchini na nje ya nchi.
RC Paul Makonda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...