Waziri wa Ardhi, Nyumba Maendeleo na Makazi Mhe. William Lukuvi leo amezindua Mpango wa kutambua na kusajili kila kipande cha Ardhi Mijini  ambapo licha ya mpango huo kuwawezesha wananchi kutumia leseni za Makazi kama dhamana ya kuchukulia mikopo pia itawawezesha kutambulika kama wamiliki halali wa maeneo yao.

Waziri Lukuvi amesema Mpango huo wa kutoa Leseni na Makazi ni mkakati wa serikali kuwakwamua wananchi kiuchumi ambapo mwananchi atahitajika kuchangia kiasi cha Shilingi 5,000 pekee ili kupata leseni ya makazi kwa Muda wa miaka mitano na baada ya hapo mwananchi atapatiwa Hati ya makazi kwakuwa tayari atakuwa anatambukika na serikali.

Kwa upande wake Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo amesema anaamini kwa utendaji mzuri wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda mpango huo unaenda kufanyika kwa ufanisi mkubwa na kuleta manufaa kwa wananchi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema mpango huo ni zaidi ya ufumbuzi na utatuzi wa kero ya migogoro ya ardhi iliyokuwa ikitumika kama kichaka cha wajanja wenye pesa kuwakandamiza wananchi wanyonge kwa kuwapora maeneo yao jambo ambalo ameahidi kulisimamia kidete.

Aidha RC Makonda amewataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kuwa na leseni za makazi kwakuwa hadi sasa takriban 70% ya maeneo ya jiji hilo hayana hati wala leseni za makazi ambapo amewataka watendaji wa kata na mitaa kutoa ushirikiano wa kutosha wataalamu wa ardhi watakaokuwa wakipita kwenye mitaa kuanzia wiki ijayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...