Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo

……………………………………………………

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa siku saba kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, kuhakikisha anaunda timu ya uchunguzi ili kuwabaini wadaiwa wa shilingi bilioni 1.34 za makusanyo ya mapato ya ndani ya halmashauri na kuwachukulia hatua wahusika wote ili kuleta ustawi katika utekelezaji wa majukumu ya kiserikali.

Amesema hayo baada ya kupitia taarifa za makusanyo na kubaini tatizo la kutowasilishwa kwa makusanyo ya mapato ya ndani kwa kutumia mfumo wa Local Governent Revenue Collection Information System (LGRCIS) na kueleza kuwa kumekuwa na watendaji ambao sio waaminifu wanaokabidhiwa makusanyo hayo na kuyaingiza kwenye matumizi binafsi wakitegemea kurudisha na matokeo yake Bili za wakusanyaji hazikubali kutoka kwenye mfumo hadi fedha zote alizokusanya zitimie.

Akitolea mfano halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mh. Wangabo alisema kuwa “hadi kufikia mwezi Februari mwaka 2019, jumla ya Shilingi Milioni 98 zimetumika kama sehemu ya gharama za wakusanyaji baada ya kuzikata na kutumia. Matokeo yake fedha zinapelekwa Halmashauri zikiwa pungufu na kuongeza kuwa jumla ya shilingi 241 za halmashauri hiyo zilitumika kabla ya kupelekwa benki jambo hilo ni kinyume na kifungu cha 32 cha Memoranda ya Fedha za Serikali za Mitaa.”

Alitoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo elekezi kwa waheshimiwa madiwani kutoka katika halmashauri zote nne za Mkoa wa Rukwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga ambapo Mh. Wangabo alikuwa mgeni rasmi wa semina hiyo.

Akitoa neno la Shukurani kwa mgeni rasmi mstahiki Meya wa manispaa ya Sumbawanga alipongeza juhudi za mkuu wa mkoa wa Rukwa kuhakikisha anasimamia vyema maendeleo ya mkoa huo, na kumuhakikishia kuwa hawatamuangusha katika kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unaongezeka

“ Sisi kama ALAT mkoa na nipende kuwaarifu madiwani wa halmashauri zote na itakuja kwenye vikao vyenu, tuliona kuliko kulalamika kwa kusema hatuna vyanzo vya mapato, halmashauri za mkoa wa Rukwa zina migogoro mingi ya ardhi kwa kutopanga matumizi ya ardhi, hivyo tumeamua ardhi zote ndani ya mkoa zipimwe na tumeshanunua mashine ya Alat K yenye thamani ya Shilingi Milioni 37 ili tuongeze mapato kwa kupima ardhi,” Alisema.

Hadi kufikia tarehe 12 mwezi Machi mwaka 2019 Manispaa ya Sumbawanga in wadaiwa wa makusanyo ya mapato ya ndani shilingi milioni 45.97, Sumbawanga Vijiji Shilingi Milioni 756.17, Wilaya ya Kalambo Shilingi Milioni 252.64 na Wilaya ya Nkasi Shilingi Milioni 290.95

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...