Na Tiganya Vincent
SERIKALI imesema inatafuta fedha kwa ajili ya kukarabati maeneo yote yaliyopo Tanzania ambayo yaliyotumika katika harakati za kudai uhuru na ukombozi katika nchi mbalimbali barani Afrika ili kutunza historia yake isipotee.
Kauli hiyo imetolewa jana Wilayani Kaliua  na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika ikiwemo eneo la Shujaa wa Afrika Mashariki na Kati Mtemi Mirambo.
Waziri alisema kuwa lengo ni kutaka historia ya mashujaa na maeneo waliyotumia isipotee ili kuwafanya  vijana wa sasa na vizazi vijavyo viwe na ukweli wa historia za mashujaa wote.
Alisema ukarabati huo unakwenda sanjari na kutafuta kumbukumbu zote walizotumia  wapigania uhuru mbalimbali kwa ajili kuzitambua na kuzihifadhi rasmi kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo ili kulinda historia isije ikapotea.
Dkt. Mwakyembe alitoa wito kwa watanzania wote wenye taarifa za kumbukumbu mbalimbali zikiwemo picha, vitabu, mashairi, nyimbo, barua na nyaraka mbalimbali zilizotumiwa na wapigania uhuru wa Tanzania na nje ya Nchi kuwasilisha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo au kwa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ili ziweze kutunzwa kwa ajili ya manufaa ya Nchi na bara la Afrika kwa ujumla.
Aidha aliwataka wananchi na Viongozi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanalinda alama zote zilizopo katika maeneo yaliyotumiwa na wapigania uhuru ikiwemo majina katika makaburi na majengo ili kutopotezakumbukumbu za mashujaa.
Katika hatua nyingine, Waziri huyo aliwataka wataalamu mbalimbali wakiwemo Maafisa Utamaduni kuhakikisha wanatumia hazina ya wazee waliopo ambao wanajua historia ya kweli kuhusu harakati za kudai uhuru nchini na mapambano ya ukombozi barani Afrika kupata maelezo na kuyaandika kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ili zisitoweke.
“Tunajua kila mtu atakufa hivyo ni vema tukatumia hazina ya wazee wetu waliopo sasa kupata historia ya kudai uhuru na harakati za ukumbozi zilizofanyika nchini ili kuweka kumbukumbu zote” alisema.
Alisema simulizi ya wazee ni muhimu katika kuhakikisha hakuna mashujaa walioshiriki harakati za kudai uhuru na ukombozi wa bara la Afrika watakaoachwa katika kumbukumbu za historia.
 Mtemi Mirambo wa II (Salumoni Kazikwa) (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe (kulia) kuhusu makaburi mbalimbali  ya ndugu zake Shujaa wa Afrika Mashariki na Kati Mtemi Mirambo wakati wa ziara yake jana ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.
 Mtemi Mirambo wa II (Salumoni Kazikwa) (mwenye kanzu nyeusi) akimwonyesha  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe (aliyevaa mgolole mweusi) choo kilichotumiwa na Shujaa wa Afrika Mashariki na Kati Mtemi Mirambo wakati wa ziara yake jana ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika ikiwemo eneo la Shujaa wa Afrika Mashariki na Kati Mtemi Mirambo.
 Mtemi Mirambo wa II (Salumoni Kazikwa) (kushoto) akimwongoza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe (kulia) kutoka nje ya makaburi mbalimbali  ya ndugu zake Shujaa wa Afrika Mashariki na Kati Mtemi Mirambo wakati wa ziara yake jana ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika ikiwemo eneo la Shujaa wa Afrika Mashariki na Kati Mtemi Mirambo.
 Mtemi Mirambo wa II (Salumoni Kazikwa) (mwenye kanzu nyeusi) akitoa maelezo kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe (aliyejifunga mgolole mweusi) kuhusu kisima kilichotumiwa Shujaa wa Afrika Mashariki na Kati Mtemi Mirambo wakati wa ziara yake jana ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika ikiwemo eneo la Shujaa wa Afrika Mashariki na Kati Mtemi Mirambo.
 Mti uliotumiwa na Shujaa wa Afrika Mashariki na Kati Mtemi Mirambo kama Mahakama wakati wa utawala wake.
 Mtemi Mirambo wa II (Salumoni Kazikwa) (mwenye Kanzu nyeusi) akimwonyesha  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe (aliyejifunga mgolole mweusi) mabaki ya Ghorofa la Shujaa wa Afrika Mashariki na Kati Mtemi Mirambo ambalo limetitia . Waziri alipata maelezo hayo wakati wa ziara yake jana ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.
 Mtemi Mirambo wa II (Salumoni Kazikwa) (mwenye Kanzu nyeusi) akimwonyesha  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe (aliyejifunga mgolole mweusi) mabaki ya Ghorofa la Shujaa wa Afrika Mashariki na Kati Mtemi Mirambo ambalo limetitia . Waziri alipata maelezo hayo wakati wa ziara yake jana ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.
 Mtemi Mirambo wa II (Salumoni Kazikwa) (aliyechuchumaa) akimwombea Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe (aliyekaa kwenye kigoda) kwenye kaburi la Shujaa wa Afrika Mashariki na Kati Mtemi Mirambo wakati wa ziara yake jana ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika ikiwemo eneo la Shujaa wa Afrika Mashariki na Kati Mtemi Mirambo.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akizugumza na wananchi kwenye Ikulu ya Shujaa wa Afrika Mashariki na Kati Mtemi Mirambo wakati wa ziara yake jana ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika ikiwemo eneo la Shujaa wa Afrika Mashariki na Kati Mtemi Mirambo.  Picha na Tiganya Vincent

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...