Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
SERIKALI imeshauriwa kuwekeza fedha nyingi kwa ajili ya kusaidia Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT), ili kukiwezesha chuo hicho kuzalisha wataalamu wa ndani watakaojenga viwanja, reli na kupata madereva wa treni na utengenezaji wa mabehewa.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayofanywa na NIT  leo Machi 16.2019  jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Moshi Kakoso amesema,  chuo hicho kimekuwa kikifanya ubunifu mkubwa utakaoleta mapunduzi kwa maendeleo ya nchi.

Amesema, pamoja na kazi nzuri wanayoifanya  ya kuzalisha wataalamu katika sekta hiyo, lakini bado  wanakabiliwa na  changamoto ya fedha ambayo serikali inapaswa kuitatua ili kuongeza ubunifu katika vitu mbali mbali.

Amesema, kama serikali itaweekeza fedha nyingi kwa ajili ya bunifu zinazofanywa na wanachuo hicho, basi hakutakuwa na haja ya kuwapeleka wakufunzi nje ya nchi ili kupata mafunzo badala yake tutakuwa tumezalisha wataalamu wetu wa ndani, na kuipunguzia nchi ya Tanzania garama kubwa.

"Uwekezaji mkubwa utasaidia kupata wataalamu watakaojenga reli ya kati, ujenzi wa meli, kukarabati mabehewa na vichwa vya treni", amesema Kakoso


Amesema, mtaalamu mmoja akipelekwa nje ya nchi hutumia Sh milioni 300 garama ambayo ni kubwa saba tunapaswa kuipunguza  sisi wenyewe kuwekeza hapa nchini  ili tupate wataalamu wa kutosha  kuliko kusubiri wanaotoka nje ya nchi ambao gharama yao ni kubwa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (anayeshughulikia Uchukuzi na Mawasiliano), Atashasta Nditiye amesema serikali imetoa kipaumbele kwa sekta ya uchukuzi na usafirishaji hivyo zimekuwa tegemezi nchini.

Nditiye amesema kupitia chuo hicho pekee Afrika Mashariki na Kikanda, kuna malengo makubwa ya kuhakikisha kuwa chuo kinazalisha wataalamu wengi watakaosaidia ujenzi wa reli ya kati, wahudumu ndani ya ndege, wahudumu katika mabehewa na madereva wazuri wa treni.

Ameongeza, serikali imeingia dhamana ya kutekeleza miradi mikubwa miwili inayofanywa chuoni hapo ambayo ni mkopo wa Benki ya Dunia (WB) na kutoka China ikiwa na lengo la kuwezesha shule ya mamlaka ya anga.

Naye Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Zacharia Mganilwa amesema miradi hiyo miwili ambayo serikali imewadhamini ni mikopo ya masharti nafuu ambapo  WB imetoa Sh bilioni 50.
Alisema fedha hizo ni maalum kwa ajili ya kuwafundisha wataalamu wa anga, marubani, wahandisi, wahudumu wa ndege, wataalamu wa masoko na menejimenti ya anga.

Pia alisema mkopo uliotolewa na China ambao ni Sh bilioni 150, unalenga kukisaidia kuwa Chuo Kikuu cha  Kikanda kwa kutoa mafunzo ya reli, kuboresha wahandisi wa relii, wahudumu, Mawasiliano na menejimenti ya usafiri wa reli ya kisasa. Aidha amesema, chuo kinatarajia kuanza kutoa mafunzo ya sayansi ya bahari na eneo kutoka mkoani Lindi limepatikana  ambako watakuwa wanajenga meli na kufanya matengenezo. Huku kwa upande wa usafiri wa anga, wataalamu tunawazalisha kwa gharama nafuu," alieleza Profesa Mganilwa.

"Tunazidi kuwahamasisha wasichana kusoma masomo ya sayansi ili wajiunge nasi katika sekta hii ya usafirishaji kwani hivi sasa ni asilimia 35 tu ya wanawake ambao wanachukua masomo haya chuoni hapa," alieleza. Kamati hiyo ilitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo kuona gari yenye uwezo wa kutembea  umbali wa kilometa 90 bila kutumia mafuta na Kitengo kinachoshughulikia masuala ya anga na urubani.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Moshi Kakosa akizungumza na  waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara ya siku moja ambapoh wametembelea miradi mbali mbali ya chuo cha NIT na  kukagua maendeleo na changamoto  katika chuo cha hicho leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji NIT,  Profesa Zacharia Mganilwa, akiwaeleza waandishi wa habari mafanikio na changamoto za miradi mbali mbali inayofanywa na chuo hicho cha NIT, wakati wa ziara ya Kamati ya ya kudumu ya binge ya Miundombinu.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Moshi Kakosa aliyekaa kulia akikagua gari lililotengenezwa na wahitimu wa Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT),  wakati wa ziara ya siku moja ya kamati hiyo shuleni iliyofanyika leo katika chuo hicho cha jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni mbunifu wa gari hilo Gabriely Jeremia na wanaoshuhudia ni baadhi ya wabunge wa kamati hiyo.
 Mbunge wa Vunjo, kupitia tiketi ya NCCR, James Mbatia akiendesha gari lililobuniwa na wahitimu wa chuo cha Usafirishaji, Gabriely Jeremia, hayupo pichani na Mtatiro Boniphace kulia wakati wa ziara ya Kamati ya ya kudumu ya bunge ya Miundombinu iliyofanyika leo chuoni hapo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...