WAZIRI Mpina akishiriki katika zoezi la uogeshaji mifugo kwenye Josho la kwanza kujengwa na Wajerumani katika nchi za Afrika Mashariki liitwalo Nunge lililojengwa mwaka 1905 lililoko wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina wa kwanza kushoto mwenye koti jeupe kwenye picha ya pamoja na wadau mballimbali mara baada ya kutoa hotuba ya tathmini ya zoezi la uogeshaji kitaifa iliyofanyika kwenye josho la kwanza kujengwa na Wajerumani katika nchi za Afrika Mashariki liitwalo Nunge lililojengwa mwaka 1905 lililoko wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.



NA JOHN MAPEPELE, MPWAPWA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amepiga marufuku mtu yoyote kutangaza kuwepo magonjwa ya mifugo nchini isipokuwa yule aliyepewa mamlaka hayo kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na taratibu za nchi na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika.

Akizungumza hivi karibuni katika tathmini ya kampeni ya uogeshaji kitaifa iliyofanyika kwenye josho la kwanza kujengwa na Wajerumani katika nchi za Afrika Mashariki liitwalo Nunge lililojengwa mwaka 1905 lililoko wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina alisema Sheria za kimataifa na Sheria ya Magonjwa ya Mifugo Namba 17 ya mwaka 2003 inazuia kufanya hivyo.

Kwenye tathmini hiyo ya miezi mitatu kuanzia Novemba 2018 hadi Februari 2019 jumla ya Mifugo milioni 32 sawa na asilimia 56 ya mifugo milioni 57 iliyopo nchini iliogeshwa ambapo kati ya mifugo iliyoogeshwa ng’ombe milioni 19.9, mbuzi milioni 8.9, kondoo milioni 2.88, punda 224 na mbwa 229,000 huku majosho yanayofanya kazi nchini ni 1,197 kati ya majosho 2,300 lakini majosho 1,124 ni mabovu hayafanyi kazi vikundi 847 vimeundwa na kufungua akaunti vikundi 612


Aidha Mpina alisisitiza kuwa shabaha ya kuzuiwa kufanya hivyo kwa sababu baadhi ya watu wanaweza kujitokeza kupeleka hofu kwa wananchi na kusababisha kuharibu biashara hiyo na hivyo mwenye dhamana ya kufanya hivyo ni Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo na sio mtu mwingine yoyote yule.

Hivyo Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo ndiye aliyepewa dhamana ya kutangaza ugonjwa wowote wa mifugo kwa niaba ya watanzania na wala sio mtendaji yoyote yule wa Serikali

Alisema nchi yetu imejipanga vizuri kudhibiti magonjwa ya mifugo na ndio maana inazo kanda nane za uchunguzi wa magonjwa ya mifugo hivyo watanzania wako salama Tanzania iko huru na magonjwa na sasa tunazalisha chanjo 8 kufikia mwezi 9 hadi mwakani kutakuwa na chanjo 11 ili mifugo ichanjwe isipatwe tena na magonjwa.

Hivyo Waziri Mpina ilifakapo Julai mosi mwaka huu wizara yake itakuwa imeshatoa kanuni za namna ya uendeshaji wa zoezi la uogeshaji ili kila mmoja afahamu wajibu wake.

Pia Waziri Mpina alisisitiza agizo lake la ukarabati wa majosho na kwamba ifikapo Julai mosi mwaka huu halmashauri ambayo itakuwa hajakarabati majosho itazuiliwa kukusanya mapato huku akizindikia barua za kusudio la kuzizuia kukusanya mapato halmashauri hizo.

Majosho 132 kati ya majosho mabovu 1,124 yameshakarabatiwa ni asilimia 11 ya agizo hilo limetekelezwa leo miezi mitatu na kuupongeza Mkoa wa Kagera ambao wamekarabati majosho 34, Mkoa wa Mwanza wamekarabati majosho 19, Mkoa wa Arusha majosho 11 wengine hawajafanya hivyo

Mpina alisema halmashauri zote nchini zinakusanya zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa mwaka mapato yanayotokana na sekta ya mifugo lakini ni halmashauri chache zinazotenga fedha kidogo za kusaidia mifugo huku Mkoa wa Dodoma hadi sasa umekarabati majosho mawili tu

Alisema mwongozo unaelekeza asilimia 15 ya mapato yanayokusanywa kutoka kwa wafugaji iende kutoa huduma kwa mifugo ikiwemo ukarabati wa majosho, malambo na chanjo hivyo lazima fedha zitengwe kwenda kwa wafugaji.

Hivyo Waziri Mpina aliziagiza Mamlaka zote zinazosimamia zoezi la uogeshaji kusimamia mwongozo uliotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikiwa ni pamoja na kila josho kuwa na kikundi na kiwe kimefungua akaunti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...