Dar es
Salaam. Shabiki wa Simba na mkazi wa mkoa wa Songwe, Willy Mwakapembe Wadson ameshinda
Sh 123,614,160 baada ya kubashiriki kwa usahihi jumla ya mechi 12 katika za mchezo wa kubahatisha wa Perfect 12
unaondeshwa na kampuni ya M-Bet Tanzania.
Mwakapembe
ambaye ni mfanyabiashara ndogondogo na mkulima wa Tunduma anakuwa mshindi wa
tatu tokea kuanza mwaka huu kushinda kiasi kikubwa cha fedha ambacho
amesema kitabadili maisha yake.
Washindi
wengine ni Frank Kayombo ambaye
alishinda kiasi cha Sh milioni 188.4 wakati mshindi wa pili alikuwa Simon Muray
aliyeshinda Sh milioni 81.
Meneja
Masoko wa M-Bet, Allen Mushi pia alisema
kuwa kuna washindi wengi waliojishindia mamilioni kupitia Jackpot Bonus ya
kampuni yao.
Mushi amesema
kampuni yao inazidi kupata washindi na mpaka sasa jumla ya Sh milioni 500
zimetumika kuwazawadia washindi mbalimbali.
Alisema kuwa
kampuni yao inazidi kuwabadili maisha Watanzania huku wakichangia pato la
serikali kiasi cha Sh milioni 24.7. Alisema ili kuweza kucheza bahati nafasi hiyo
unaweza kutembelea http://bit.ly/2VZCB38
ili kuanza kuanza kubet.
“M-Bet
inazidi kuchanja mbuga na kuinua vipato vya Watanzania na kuchangia maendeleo
ya nchi chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dk John Pombe Joseph Magufuli.
Nawaomba Watanzania kucheza ili kushinda
zawadi za fedha,” alisema Mushi.
Akizungumza mara
baada ya kukabidhiwa fedha zake, Wadson alisema kuwa alianza kubeti muda mrefu
kabla ya kupata ushindi huo mnono.
Alisema kuwa
hakukata tamaa pamoja na kutaniwa na marafiki zake wengi kuwa hataweza kushinda
fedha nyingi zaidi ya kupoteza muda wake.
“Sikukata
tamaa na kuendelea kubeti, niliamini kuwa siku moja nitapata bahati ya
kushinda, nashukuru Mungu kupata kiasi hiki cha fedha na nitakaa mke wangu
kupanga jinsi gani ya kuwekeza na kujiongezea kipato,” alisema Mwakapembe.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (Kulia) akikabidhi mfano wa
hundi, Willy Mwakapemba (katikati)
kutoka mkoa wa Songwe aliyeshinda Sh Milioni 123.7 za mchezo wa Perfect 12 wa
kampuni ya M-Bet Tanzania. Anayeshuhudia ni Kaimu Msimamizi wa Kitengo cha Michezo ya
Kubahatisha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi, Ilala Philipo
Haule.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...