TIMU ya Taifa ya walemavu wa akili, wanatarajia kuwasili nchini leo mchana ikiwa na medali 15 kutoka katika michezo ya Dunia ya walemavu wa akili iliyomalizika Falme za Kiarabu (UAE).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Special Olympics Tanzania (SOT), Charles Rays katika medali hizo, 12 za dhahabu, fedha moja na Shaba 2 zilizopatikana katika Riadha na Mpira wa Wavu.

Rays alisema michezo hiyo iliyochezwa UEA, michezo ya Riadha ilichezwa Abu Dhabi huku Mpira wa Wavu michezo hiyo ilifanyika Dubai.

Katika mpira wa Kikapu, Tanzania imeibuka mabingwa baada ya kuiadhibu Italia kwa seti 2-1 katika fainali.

Rays alisema katika riadha Tanzania imezoa medali 9 za dhahabu , Fedha moja na shaba 2 ambako Boniventura Anga wa Mtwara alipata medali ya dhahabu.

Aidha katika michezo hiyo, Tanzania ilishiriki michezo hiyo sambamba na wachezaji kutoka kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nyarugusu.

Katika mapokezi hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Alex Nkenyenge anatarajia kuwapokea wanamichezo hao ambao wameiletea heshima Tanzania katika michezo hiyo.

Michezo ya dunia ya majira ya kiangazi yalianza Machi 14 na kumalizika Machi 21 (UAE).


  Mwanariadha Boniventura Anga kutoka Mtwara akionesha medali yake ya dhahabu baada ya kufanya vizuri katika michezo ya dunia iliyomalizika Falme za Kiarabu.
 Picha ya pamoja
 Mkurugenzi wa Special Olympics International (SOI), Tim Shriver akipunga mikono juu na timu ya Taifa ya Tanzania katika michezo ya dunia nchini UAE



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...