KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd leo Machi 13, imetangaza rasmi  ujio wa tamthiliya mpya ya kihindi iliyotafasiriwa na kuingiziwa sauti za Kiswahili hapa nchini.

Tamthiliya ya Waaris ikiwa na maana ya  Mrithi kwa kiswahili  inakuwa  tamthiliya ya kwanza kwenye kingamuzi cha StarTimes kwa kuingizwa sauti za Kiswahili hapa nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meneja masoko wa Startimes Davis Malisa amesema kuwa katika kuhakikisha wateja wao wanapata burudani wanayostahili, StarTimes kupitia chaneli ya ST Swahili wataanza kuonyesha tamthiliya hiyo siku ya Alhamisi tarehe 14 Machi mwaka huu.

“Tunaendelea kujipambanua kama wafalme wa burudani za kifamilia, na tamthiliya hii mpya ina maudhui ambayo yanaweza kuangaliwa na familia na itaanza kuonekana kwenye chaneli yetu ya StarTimes Swahili siku za Alhamisi na Ijumaa kuanzia saa 2:30 hadi saa 3:30 Usiku" ameeleza David.

Imeelezwa kuwa tamthiliya ya Waaris inazungumzia masuala ya malezi na matokeo ya malezi hayo pamoja na mambo mengine. Pia inaonyesha unyanyasaji wa kijinsia ambao pia bado ni changamoto katika jamii zetu, bila kusahau uhalisia wa ambavyo kina mama wanawalinda watoto wao. 

Baadhi ya waigizaji walioshiriki  kuingiza sauti za Kiswahili katika tamthiliya hiyo ya Warris ni pamoja na  Yvonne Cherry (Monalisa), Godliver Gordian, Sophie na Rakheem David ambao wameonesha uwezo wa hali ya juu katika kuingiza sauti na kwa ujumla wameitendea haki Waaris.

Tamthiliya hiyo itaonyeshwa na chaneli ya ST Swahili pekee ambayo inapatikana katika kifurushi cha Nyota kwa gharama ya shilingi 8000 na kwa watumiaji wa Antenna na gharama ya shilingi 11,000 kwa watumiaji wa dikoda za Antenna.

Meneja masoko wa Startimes Davis Malisa  akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kuonesha tamthiliya mpya ya kihindi iliyotafasiriwa na kuingiziwa sauti za Kiswahili itakayokuwa inaoneshwa kupitia kwenye kingamuzi cha Startimes leo uliofanyika katika ukumbi wa sinema uliopo mlimani City jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...