Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA  ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), leo imetoa ya misahafu 29 kwa Madrasat-ul-Istiqama ya Buguruni, Mtaa wa Ghana, jijini Dar es salaam kwa ajili ya watoto wanaosoma elimu ya dini ya Kiislam.
Akikabidhi vitabu hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Kaimu Mkurugenzi wa Uhandisi na Huduma za Ufundi, Mhandisi Mbila Mdemu amesema mbali na kazi za kuendesha, kusimamia na kuendeleza Viwanja vya Ndege Tanzania Bara, TAA imekuwa ikishirikiana na jamii katika masuala mbalimbali yanayohusu jamii.
Mhandisi Mdemu amesema pamoja na kwamba Madrasat hiyo ina watoto takribani 230, lakini anaamini wataweza kupokezana vitabu hivi na kupata mafunzo yaliyo sahihi, yatakayowajengea malezi bora yenye msingi wa amani na mshikamano.
Amesema msaada huu wa vitabu vya dini utasaidia kuanza kuwaandaa watoto hao, ambao baadaye wakiwa wakubwa wanakuwa ni sehemu ya jumuiya na sehemu ya Mamlaka na jamii nzima ya Kitanzania, ambapo watakuwa waadilifu na wenye maadili mema kwa taifa kwa kuwa wamepata msingi mzuri wa elimu ya dini, ambao ndio chimbuko la uadilifu na amani.
“Hii ni kawaida ya Mamlaka kutoa misaada kwa jamii, na ninaamini msaada huu pia utasaidia kufanya kitu kikubwa katika jamii yetu, kwa kuwa watoto hawa ndio watakuja kuwa watumishi wa miaka ijayo, hivyo watakuwa mfano wa kuigwa katika jamii,” amesema Mhandisi Mdemu.
Pia Mhandisi, amewakaribisha kutembelea TAA kwa ajili ya kujifunza na kuwa na ari ya kufanya kazi na Taasisi hii, ambayo ipo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi).
Naye Katibu wa Madrasat hiyo, Hemed Suleiman ameishukuru TAA kwa kujitoa kwao kwa kutoa msaada huo, ambao ni moja ya vitu muhimu kwao.
“Nawashukuru sana tena sana kwa msaada huu, hatuna cha kuwalipa ila Mungu awazidishie pale mlipotoa, muendelee kuwasaidia watu zaidi ya sisi” ameshukuru Bw. Suleiman.

 Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhandisi na Huduma za Ufundi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Mbila Mdemu (kushoto), leo akimkabidhi Katibu wa Madrasat-ul-Istiqama, Ustaadh Hemed Suleiman misahafu 29, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa wa Mamlaka hiyo, Richard Mayongela.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakishughudia Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhandisi na Huduma za Ufundi, Mhandisi Mbila Mdemu (kushoto) akikabidhi Katibu wa Madrasa ya Istiqama ya Buguruni, Ghana, Ustaadh Hemed Suleiman moja ya misahafu 29 waliyotoa msaada leo.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...