Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea na Semina kwa wajasiliamali wadogo katika Wilaya ya Lushoto ya kutoa Elimu kwa walengwa, kuhusu utekelezaji wa viwango vya kitaifa vya bidhaa zinazozalishwa na zinazosindikwa, pamoja na namna ya kupata alama ya ubora kwenye bidhaa wanazozalisha,Sambamba na jinsi gani wajasiriamali wanaweza kupata Leseni ya TBS bure bila gharama yoyote.

Semina hiyo kwa wajasiliamali wadogo imefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, huku wajasiriamali 33 wakijitokeza kupata elimu hiyo sambamba na ufahamu wa masuala mbalimbali yahusuyo Ubora wa Bidhaa. Wajasiriamali hao wanazalisha bidhaa za maziwa, siagi, mtindi, asali, jam, juisi, mbogamboga, wasindikaji wa nyanya na vitunguu saumu.

TBS katika semina hizi inashirikiana na taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) na ofisi ya Afisa Biashara.

Akifungua Semina hiyo Mhe. January Lugangika, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, amesisitiza washiriki kutumia hii fursa kwa kusikiliza kwa makini ili kutumia elimu watakayopata katika kuzalisha bidhaa zenye ubora unaotakiwa, kwani vita dhidi ya umaskini ni yetu sote. Aidha Mh. January ameongeza kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda ni lazima kuzingatia viwango kwani vita dhidi ya umaskini ni yetu sote.

Akifunga semina hiyo, Afisa Udhibiti Ubora Mkuu, Cunbert Kapilima (TBS), alisisitiza kuwa TBS inatambua mchango wa wajasiriamali katika kukuza pato la taifa na kutengeneza ajira kwa wananchi walio wengi. Hivyo TBS ina mchakato endekevu kutoa elimu kwa wajasiliamali kwa kuwa ni mojawapo ya majukumu yake ya kila siku. 

TBS mpaka sasa imeshatoa semina na mafunzo kwa bidhaa mbalimbali kwa washiriki kutoka mikoa ya Dodoma, Singida, Katavi, Kagera, Kigoma, Tanga, Tabora, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa, Njombe, Songwe, Rukwa, Mbeya, Mwanza na Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya  Lushoto, Mhe. January Lugangika akifungua Semina ya wajasiliamali katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya Lushoto, Machi 18, 2019. Kushoto ni Bw. Cunbert Kapilima, Afisa udhibiti ubora mkuu(TBS) na kulia ni   Bw. Faustine January, Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kaskazini (TBS).
 Bi. Gladness Foya, Afisa maendeleo ya biashara (SIDO), akiwasilisha mada ya teknolojia za usindikaji bidhaa za vyakula kwa wajasiliamali wa Wilaya ya  Lushoto.
Bw. Cunbert Kapilima, Afisa udhibiti ubora mkuu(TBS), akiwasilisha mada ya elimu ya ufungashaji kwa wajasiliamali wa Lushoto (w).
 Bw.Halfa Sume, Mkaguzi wa Chakula (TFDA), akiwasilisha mada ya usajili wa jengo na bidhaa za chakula kwa wajasiliamali wa Lushoto (W).
 Wajasiliamali wilayani Lushoto (W), wakisikiliza mada mbalimbali katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya lushoto.
Bw.Stephen Rwabunywenge, Afisa Viwango Mwandamizi (TBS), akiwasilisha mada ya viwango vya chakula, matumizi na faida za viwango kwa wajasiliamali wa Lushoto (W).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...