Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu kwa waagizaji wa bidhaa mbalimbali na wakala wa forodha katika mpaka wa Horohoro na bandari ya Tanga  juu ya utaratibu na mifumo ya ukaguzi wa bidhaa mbalimbali kabla hazijaingia nchini " Pre- shipment Verification of Conformity (PVoC)", ukaguzi wa bidhaa baada ya kuwasili nchini "Destination Inspection (DI)", uthibitishaji wa bidhaa na matakwa ya viwango.

Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa ofisi za Bandari na  washiriki 33 walihudhuria. Semina hii ilifunguliwa na Thobias Mwilapwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, ambaye alisisitiza washiriki kusikiliza kwa makini taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili kuepuka gharama ya kupoteza muda na pesa, kwa kutokufuata taratibu au kuingiza bidhaa zilizochini ya kiwango.
 
Baadhi ya washiriki wakati wa majadiliano, waliomba TBS kuhakikisha majibu ya sampuli yanatoka kwa haraka ili kuepuka gharama za ziada ya kuhifadhi mizigo yao. Kwa upande wake Gladness Kaseka, Afisa Masoko Mwandamizi (TBS), aliwasisitiza washiriki kuwa na hulka ya kutuma malalamiko yao rasmi kwenye dawati la huduma kwa mteja, kupitia namba ya bure ambayo ni 0800110827, ili yaweza kushughulikiwa kuliko kubaki nayo na kusubiri mikutano au semina.

TBS imeendelea kutoa semina kama hizi kwa waagizaji bidhaa mbalimbali na mawakala wa forodha mkoani Mwanza na Dar es Salaam, na hivi karibuni itatolewa pia katika mkoa wa Arusha.
 Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa akifungua Semina kwa waagizaji wa bidhaa mbalimbali na mawakala wa forodha katika Bandari ya Tanga na Horohoro, katika ukumbi wa Bandari , Machi 20, 2019. Kushoto ni Bw. Cunbert Kapilima, Afisa Udhibiti Ubora Mkuu(TBS) na kulia ni   Bw. Faustine January, Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kaskazini (TBS).
Afisa viwango mwandamizi (TBS), Stephen Rwabunywenge akiwasilisha mada ya matakwa ya msingi wa viwango kwa waagizaji wa mizigo na mawakala wa forodha  katika bandari ya Tanga na Horohoro.
Afisa Udhibiti Ubora (TBS), Emmanuel Kiwango akiwasilisha mada juu ya utaratibu wa kufuatwa kwa mizigo inayoingizwa bila kukaguliwa inapotoka na kukaguliwa nchini " Destination Inspection" kwa waagizaji na mawakala wa forodha katika bandari ya Tanga na Horohoro.
 Waagizaji mizigo na mawakala wa forodha katika bandari ya Tanga na mpaka wa Hororo, wakiwa pamoja na watoa mada wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Thobias Mwilapwa(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi.
 Afisa Udhibiti Ubora (TBS), Bi. Janeth Kakuru akiwasilisha mada ya ukaguzi wa bidhaa katika nchi zinakotoka kabla hazijasafirishwa kuja hapa nchini (PVoC),kwa waagizaji na mawakala wa forodha mkoani Tanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...