Na Chalila Kibuda Globu ya Jamii.

Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya Mashariki imesema kuwa njia ya bora ya kufanya watumiaji wa mawasiliano kufuata sheria na taratibu za mawasiliano hayo ni kuwapa elimu.

Hayo aliyasema Mkuu wa Kanda ya Mashariki Mhandisi Lawi Odiero wakati wa maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mlaji Duniani ambapo Kanda hiyo ilitoa elimu katika shule ya Sekondari Minaki iliyopo Kisarawe mkoani Pwani amesema wanafunzi wa kidato cha Tano na Sita ndio wanaingia katika utumiaji wa mawasiliano hivyo lazima wapewe elimu ya kutosha katika kutumia mawasiliano hayo.

Odiero amesema wanafunzi wakipata njia bora ya utumiaji wa mawasiliano wanakuwa chachu katika kuelimisha watu wengine kutokana na uelewa wao kuwa mkubwa.Amesema katika maadhimisho ya siku ya haki ya walaji duniani inatoa fursa katika TCRA kuwa na muendelezo ws kutoa elimu ya mawasiliano kwa wadau ili wajue sharia mbalimbali za mawasiliano hayo ili yasitumike visivyo na kuondoa maana ya mawasiliano.

Amesema katika kuelekea uchumi wa viwanda mawasiliano ni njia ya kufungua fursa ya watumiaji wa mawasiliano hayo kutengeneza ajira kutokana na teknolojia iliyopo katika mitandao ya simu.Aidha amesema kuwa sheria iliyopo kwa kampuni za simu ni kuhakikisha wanatoa huduma bora ya mawasiliano na wale ambao wanakiuka sheria kushika mkondo wake.

Amesema watumiaji wa mawasiliano wanatakiwa kutuma ujumbe wenye maadili na wanaofanya kutuma ujumbe wa uchochezi,matusi kufunguliwa mashitaka mahakamani lengo ni kufanya mawasiliano kuwa salama.

"Dunia hii imekuwa kijiji kutokana na mawasiliano hivyo kila kitu kinachofanyika kiendane na maadili yetu nchini pamoja na watu wengine wajifunze kwani sio kila kitu kiwekwe katika mawasiliano na njia rahisi kila mtu anayepata ujumbe usiofaata maadili hayo ni kufuta"amesema Odiero.

Nae Mwalimu wa Shule ya Sekondari Minaki Sweatbert Kijumba amesema wanafunzi wakipewa elimu ndio nguzo ya kufanya nchi kuwa na mawasiliano salama kwani wenyewe ndio wanaingia kwa kasi katika utumiaji wa mawasiliano.

Amesema Teknolojia ya mawasiliano inabadilika hivyo TCRA iendelee kutoa elimu katika makundi mbalimbali ili watumiaji wajue sheria za mitandao kwa kuwafikia moja kwa moja.Kwa upande wa Afisa Masoko wa TCRA Joyce Paul amesema kuwa wanafunzi wakipata uelewa wa matumizi ya simu ndio mabalozi wa kuelimisha jamii katika ngazi za familia.

 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wakati Kanda hiyo ilipokwenda kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule ikiwa ni maadhimisho ya Siku Haki ya Walaji ambayo hufanyika kila Machi 15 ya kila Mwaka.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wakiwasikiliza TCRA Kanda ya Mashariki wakati wa maadhimisho ya Siku ya Haki Mlaji Duniani ambayo hufanyika Machi 15 ya Kila Mwaka.
 Afisa Masoko wa Mamlaka ya Mawasiliano Joyce Paul akitoa maelezo kuhusiana utendaji wa mamlaka katika udhibiti wa mawasiliano wakati Kanda ya Mashariki TCRA ilipokwenda kutoa elimu katkka shule ya Sekondari Minaki iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
 Mhandisi Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki TCRA Robson Shaban akitoa maelezo namna wanavyofatilia mawasiliano wakati akitoa elimu katika Shule ya Sekondari Minaki ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Haki Mlaji Duniani.
 Mwalimu wa Shule ya Sekindari Minaki Sweatbert Kijumba akitoa maelezo juu ya ujio wa TCRA Kanda ya Mashariki katika shule hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Haki Mlaji Duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...