LAGOS, NIGERIA

TAASISI ya Hisani la Tony Elumelu Foundation (TEF), ambayo inaongoza kwa uwezeshaji wajasiriamali wa Afrika, linatarajia kutangaza majina ya waombaji waliopitishwa kushiriki programu ya ujasiriamali Machi 22, mwaka huu.

Tukio hilo, ambalo litaashiria awamu ya tano ya programu ya uwezeshaji ya shirika hilo, itafanyika kwenye Hoteli ya Transcorp Hilton Hotel, mjini Abuja Nigeria.

Kila mwaka TEF hukaribisha maombi ya uwezeshaji kwa wajasiriamali wa Afrika, wenye biashara zenye umri usiozidi miaka mitatu.

Kupitia programu yake yenye thamani ya dola milioni 100, taasisi hiyo huwezesha wajasiriamali 1,000 kila mwaka, ambao hupokea dola 5,000 kama mtaji wa kuchochea biashara zao.

Aidha hukutana na wataalamu, programu ya mafunzo ya wiki 12 na fursa za kutangaza biashara zao kwa ulimwengu wa kibiashara.

Waombaji wote hupata fursa ya kuunganishwa na mtandao wa kidijitali wa TEFConnect, ambao ni kitovu cha dijitali ya ujasiriamali barani Afrika, ukitoa fursa ya kuunganishwa na mitandao, mafunzo na vyanzo zaidi vya mitaji na fursa za kibiashara.

Katika miaka mitano tangu taasisi hiyo izindue programu ya ujasiriamali, imewezesha moja kwa moja wajasiliamali 4,000 wa Afrika na wengine 470 wakisaidiwa na wabia wa TEF.

Akizungumzia programu hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu mpya wa TEF, Ifeyinwa Ugochukwu, ambaye anachukua nafasi ya Parminder Vir, atakayebakia katika bodi ya ushauri kuanzia Aprili Mosi, mwaka huu, alisema kuna umuhimu wa kuongeza idadi ya wanufaika wa kila mwaka kutoka 1,000 ya sasa.

“Kila mwaka tunashuhudia ongezeko la waombaji hivyo idadi ya wanufaika itapaswa kuongezeka. Mbia wetu, Accenture Development Partnerships, kwa sasa anatathimini na kupitisha waombaji.

“Zaidi ya wajasiliamali 215,000 wa Afrika kutoka mataifa 54 waliwasilisha maombi likiwa ongezeko kutoka waombaji 151,000 wa mwaka jana na kutoka 62,000 mwaka 2018 hadi 90,000 mwaka 2019 kwa pande wa wanawake. “Kupanda kwa takwimu hizi kunaonesha dhamira tya mjasiriamali wa Afrika kuendeleza bara letu na tunatakiwa kugeuza dhamira hii kuwa fursa ya biashara itakayochochea maendeleo ya bara letu,” alisema Ugochukwu.
 
 Baadhi ya wajasiriamali kutoka nchi za Afrika waliohudhuria mafunzo mwaka jana
 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...